Esther 3:5 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hamani aliwaka hasira alipojua kwamba Mordekai hamwinamii wala hamsujudii.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hamani alipoona kuwa Mordekai hampigii magoti wala kumpa heshima, alighadhibika.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata Hamani alipoona ya kwamba Mordekai hainami wala kumsujudia, alighadhibika sana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hamani aliwaka hasira alipojua kwamba Mordekai hamwinamii wala hamsujudii.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati Hamani alipoona kuwa Mordekai hampigii magoti wala kumpa heshima alighadhibika.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati Hamani alipoona kuwa Mordekai hampigii magoti wala kumpa heshima alighadhibika.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hamani alipoona, ya kuwa Mordekai hampigii magoti, wala hamwangukii, ndipo, makali yenye moto yalipomjaa Hamani moyoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata Hamani alipoona ya kwamba Mordekai hainami wala kumsujudia, alighadhibika sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hamani akawaka hasira alipojua kwamba Mordekayi hainami wala kupiga magoti mbele yake.