Esther 3:6 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena alipogundua kuwa Mordekai alikuwa Myahudi, aliamua kwamba kumwadhibu peke yake haitoshi. Basi akala njama kuwaangamiza Wayahudi wote, watu wa ukoo wa Mordekai, katika utawala wa mfalme Ahasuero.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hata hivyo, baada ya kujulishwa watu wa Mordekai ni akina nani, alibadili wazo la kumuua Mordekai peke yake. Badala yake Hamani alitafuta njia ya kuwaangamiza watu wote wa Mordekai, yaani Wayahudi, walio katika ufalme wote wa Ahasuero.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaona si shani kumtia mikono Mordekai peke yake; maana wamemjulisha kabila yake Mordekai; kwa hiyo Hamani alitaka kuwaangamiza Wayahudi wote waliokuwa wakikaa katika ufalme wote mzima wa Ahasuero, yaani, watu wake Mordekai.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena alipogundua kuwa Mordekai alikuwa Myahudi, aliamua kwamba kumwadhibu peke yake haitoshi. Basi akala njama kuwaangamiza Wayahudi wote, watu wa ukoo wa Mordekai, katika utawala wa mfalme Ahasuero.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata hivyo baada ya kujulishwa watu wa Mordekai ni akina nani, alibadili wazo la kumwua Mordekai peke yake. Badala yake Hamani alitafuta njia ya kuwaangamiza watu wote wa Mordekai, yaani, Wayahudi, walio katika ufalme wote wa Ahusuero.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hata hivyo baada ya kujulishwa watu wa Mordekai ni akina nani, alibadili wazo la kumuua Mordekai peke yake. Badala yake Hamani alitafuta njia ya kuwaangamiza watu wote wa Mordekai, yaani, Wayahudi, walio katika ufalme wote wa Ahasuero.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini akaona, ya kama haimpasi kumkamata Mordekai peke yake, kwani walimwambia nao ukoo wake Mordekai; kwa hiyo Hamani akatafuta njia ya kuwaangamiza Wayuda wote pia waliokuwa katika ufalme wote wa Ahaswerosi, kwa kuwa ukoo wake Mordekai.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaona si shani kumtia mikono Mordekai peke yake; maana wamemjulisha kabila yake Mordekai; kwa hiyo Hamani alitaka kuwaangamiza Wayahudi wote waliokuwa wakikaa katika ufalme wote mzima wa Ahasuero, yaani, watu wake Mordekai.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena alipogundua kwamba Mordekayi alikuwa Muyuda, akaamua kwamba kumwazibu peke yake haitoshi. Basi akafanya shauri la kuwaangamiza Wayuda wote, watu wa ukoo wa Mordekayi, katika utawala wa mufalme Ahasuero.