Esther 3:7 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Katika mwaka wa kumi na mbili wa utawala wa mfalme Ahasuero, mnamo mwezi wa kwanza uitwao Nisani, Hamani aliagiza kura (yaani Purimu) ifanywe kupata siku na mwezi ambapo angetekeleza njama zake. Basi, kura ikaangukia siku ya kumi na nne ya mwezi wa kumi na mbili uitwao Adari.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika mwaka wa kumi na mbili wa utawala wa Mfalme Ahasuero, katika mwezi wa kwanza uitwao Nisani, walipiga puri (yaani kura) mbele ya Hamani ili kuchagua siku na mwezi. Kura ikaangukia kwenye mwezi wa kumi na mbili, yaani Adari.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi mwezi wa kwanza, ndio mwezi wa Nisani, mwaka wa kumi na mbili wa mfalme Ahasuero, wakapiga Puri, yaani kura, mbele yake Hamani; siku kwa siku, na mwezi kwa mwezi, hata mwezi wa kumi na mbili, ndio mwezi wa Adari.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Katika mwaka wa kumi na mbili wa utawala wa mfalme Ahasuero, mnamo mwezi wa kwanza uitwao Nisani, Hamani aliagiza kura (yaani Purimu) ifanywe kupata siku na mwezi ambapo angetekeleza njama zake. Basi, kura ikaangukia siku ya kumi na nne ya mwezi wa kumi na mbili uitwao Adari.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika mwaka wa kumi na mbili wa kutawala Mfalme Ahusuero, katika mwezi wa kwanza uitwao Nisani, walipiga puri (yaani kura) mbele ya Hamani kuchagua siku na mwezi. Kura ikaangukia kwenye mwezi wa kumi na mbili, yaani Adari.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika mwaka wa kumi na mbili wa utawala wa Mfalme Ahasuero, katika mwezi wa kwanza uitwao Nisani, walipiga puri (yaani kura) mbele ya Hamani ili kuchagua siku na mwezi. Kura ikaangukia kwenye mwezi wa kumi na mbili, yaani Adari.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Katika mwezi wa kwanza, ndio Nisani, katika mwaka wa kumi na mbili wa mfalme Ahaswerosi wakapiga Puri, ndio kura, machoni pake Hamani siku kwa siku, hata mwezi kwa mwezi mpaka mwezi wa kumi na mbili, ndio Adari.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi mwezi wa kwanza, ndio mwezi wa Nisani, mwaka wa kumi na mbili wa mfalme Ahasuero, wakapiga Puri, yaani kura, mbele yake Hamani; siku kwa siku, na mwezi kwa mwezi, hata mwezi wa kumi na mbili, ndio mwezi wa Adari.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika mwaka wa kumi na mbili wa utawala wa mufalme Ahasuero, katika mwezi wa kwanza unaoitwa Nisani, wakapiga Purimu, maana yake kura, mbele ya Hamani kusudi ajue mwezi na siku ya kuwaangamiza. Basi kura ikaangukia mwezi wa kumi na mbili unaoitwa Adari.