Esther 3:8 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Hamani akamwambia mfalme: “Wapo watu wa taifa fulani walioko kila mahali katika utawala wako, nao wako katika kila mkoa. Watu hao wana sheria zilizo tofauti kabisa na za watu wengine. Isitoshe, wao hawazitii sheria zako, kwa hiyo haikufaidi chochote kuwavumilia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Hamani akamwambia Mfalme Ahasuero, “Wako watu fulani wameenea na kutawanyika miongoni mwa watu katika majimbo yote ya ufalme wako, ambao desturi zao ni tofauti na zile za watu wengine wote, nao hawatii sheria za mfalme. Haifai mfalme kuwavumilia watu hawa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Hamani akamwambia mfalme Ahasuero, Kuna taifa moja waliotawanyika na kukaa mahali mahali katikati ya mataifa walioko katika majimbo yote ya ufalme wako. Nao sheria zao zimefarakana na sheria za kila taifa; wala hawazishiki amri za mfalme; kwa hiyo haimpasi mfalme kuchukuliana nao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Hamani akamwambia mfalme: “Wapo watu wa taifa fulani walioko kila mahali katika utawala wako, nao wako katika kila mkoa. Watu hao wana sheria zilizo tofauti kabisa na za watu wengine. Isitoshe, wao hawazitii sheria zako, kwa hiyo haikufaidi chochote kuwavumilia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Hamani alimwambia Mfalme Ahusuero, “Wako watu fulani wameenea na kutawanyika miongoni mwa watu katika majimbo yote ya ufalme wako, ambao desturi zao ni tofauti na zile za watu wengine wote, nao hawatii sheria za mfalme. Haifai mfalme kuwavumilia watu hawa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Hamani akamwambia Mfalme Ahasuero, “Wako watu fulani wameenea na kutawanyika miongoni mwa watu katika majimbo yote ya ufalme wako, ambao desturi zao ni tofauti na zile za watu wengine wote, nao hawatii sheria za mfalme. Haifai mfalme kuwavumilia watu hawa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Hamani akamwambia mfalme Ahaswerosi: Liko kabila moja lililotawanyika katikati ya makabila mengine katika majimbo yote ya ufalme wako, nao wanakaa na kujitenga kabisa, nayo maongozi yao ni mengine kabisa, siyo ya makabila yote mengine, nayo maagizo ya mfalme hawayafanyi. Kwa hiyo haimpasi mfalme kuwaacha, wajikalie tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Hamani akamwambia mfalme Ahasuero, Kuna taifa moja waliotawanyika na kukaa mahali mahali katikati ya mataifa walioko katika majimbo yote ya ufalme wako. Nao sheria zao zimefarakana na sheria za kila taifa; wala hawazishiki amri za mfalme; kwa hiyo haimpasi mfalme kuchukuliana nao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Hamani akamwambia mufalme: “Kuna watu wa taifa moja wanaokuwa kila nafasi katika utawala wako, nao wako katika kila jimbo. Watu hao wana sheria zinazokuwa tofauti kabisa na za watu wengine. Vilevile, wao hawazitii sheria zako, kwa hiyo haikufaidii kwa kitu chochote kuwavumilia.