Esther 4:1 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mordekai alipojua yote yaliyotukia, alizirarua nguo zake, akavaa vazi la gunia, na kujitia majivu. Kisha, akapita katikati ya mji akilia kwa sauti ya uchungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mordekai alipojua yote yaliyokwisha kufanyika, alirarua mavazi yake, akavaa magunia na kujipaka majivu, akaenda mjini akiomboleza kwa sauti na kwa uchungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Mordeikai alipojua mambo yote yaliyofanyika, alizirarua nguo zake, akajivika gunia pamoja na majivu, akatoka hata kufika katikati ya mji, akalia kwa sauti kuu ya uchungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mordekai alipojua yote yaliyotukia, alizirarua nguo zake, akavaa vazi la gunia, na kujitia majivu. Kisha, akapita katikati ya mji akilia kwa sauti ya uchungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati Mordekai alipojua yote yaliyokwisha kufanyika, alirarua mavazi yake na kuvaa nguo za magunia na kujipaka majivu, akaenda mjini, akiomboleza kwa sauti na kwa uchungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mordekai alipojua yote yaliyokwisha kufanyika, alirarua mavazi yake na kuvaa nguo za magunia na kujipaka majivu, akaenda mjini, akiomboleza kwa sauti na kwa uchungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mordekai alipoyajua hayo yote yaliyofanyika, Mordekai akazirarua nguo zake, akavaa gunia na majivu, akatokea mjini katikati, akaomboleza maombolezo makuu yenye uchungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Mordeikai alipojua mambo yote yaliyofanyika, alizirarua nguo zake, akajivika gunia pamoja na majivu, akatoka hata kufika katikati ya mji, akalia kwa sauti kuu ya uchungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mordekayi alipojua yote yaliyotukia, akapasua nguo zake, akavaa nguo ya gunia, na kujitia majivu. Kisha, akapita katikati ya muji akilia kwa sauti ya uchungu.