Esther 4:11 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Watumishi wote wa mfalme na raia wa mikoa yote wanajua ya kwamba mtu yeyote yule akiingia katika ua wa ndani na kumwona mfalme bila kuitwa, huyo ni lazima auawe. Anayeweza kunusurika ni yule tu ambaye mfalme atamnyoshea fimbo yake ya dhahabu ili kumsalimisha. Kumbe mimi sijaitwa na mfalme, yapata mwezi mzima sasa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Maafisa wote wa mfalme na watu wa majimbo ya ufalme wanajua kuwa mwanaume au mwanamke yeyote ambaye ataingia kumwona mfalme katika ua wa ndani bila kuitwa, mfalme ana sheria moja tu: Atauawa. Njia pekee kinyume na hili ni mfalme kumnyooshea fimbo ya dhahabu ili aishi. Lakini siku thelathini zimepita tangu nilipoitwa kwenda kwa mfalme.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Watumwa wote wa mfalme wanajua sana, hata na watu wa majimbo ya mfalme, ya kwamba mtu ye yote, akiwa mwanamume au mwanamke, atakayemjia mfalme katika ua wa ndani, wala hakuitwa, kuna sheria moja kwake, ni kwamba auawe; isipokuwa yeye ambaye mfalme atamnyoshea fimbo ya dhahabu, ili aishi; wala mimi sikuitwa niingie kwa mfalme yapata siku thelathini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Watumishi wote wa mfalme na raia wa mikoa yote wanajua ya kwamba mtu yeyote yule akiingia katika ua wa ndani na kumwona mfalme bila kuitwa, huyo ni lazima auawe. Anayeweza kunusurika ni yule tu ambaye mfalme atamnyoshea fimbo yake ya dhahabu ili kumsalimisha. Kumbe mimi sijaitwa na mfalme, yapata mwezi mzima sasa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Maafisa wote wa mfalme na watu wa majimbo ya kifalme wanajua kuwa mwanaume au mwanamke ye yote ambaye ataingia kumwona mfalme katika ua wa ndani bila kuitwa, mfalme ana sheria moja tu: Atauawa. Njia pekee kinyume na hili ni mfalme kumnyoshea fimbo ya dhahabu ili aishi. Lakini siku thelathini zimepita tangu nilipoitwa kwenda kwa mfalme.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Maafisa wote wa mfalme na watu wa majimbo ya ufalme wanajua kuwa mwanaume au mwanamke yeyote ambaye ataingia kumwona mfalme katika ua wa ndani bila kuitwa, mfalme ana sheria moja tu: Atauawa. Njia pekee kinyume na hili ni mfalme kumnyooshea fimbo ya dhahabu ili aishi. Lakini siku thelathini zimepita tangu nilipoitwa kwenda kwa mfalme.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watumishi wote wa mfalme na watu wote wa majimbo ya mfalme wanayajua haya: kila mtu, kama ni mwanamume au mwanamke aingiaye kwa mfalme katika ua wa ndani, asipokuwa ameitwa, hana budi kuuawa kwa ile amri moja ya mfalme; atakayepona ni yule tu, mfalme ampungiaye kwa bakora yake ya dhahabu. Nami sikuitwa kuingia kwa mfalme, sasa ni siku thelathini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Watumwa wote wa mfalme wanajua sana, hata na watu wa majimbo ya mfalme, ya kwamba mtu ye yote, akiwa mwanamume au mwanamke, atakayemjia mfalme katika ua wa ndani, wala hakuitwa, kuna sheria moja kwake, ni kwamba auawe; isipokuwa yeye ambaye mfalme atamnyoshea fimbo ya dhahabu, ili aishi; wala mimi sikuitwa niingie kwa mfalme yapata siku thelathini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Watumishi wote wa mufalme na watu wote wa majimbo yote wanajua kwamba mutu yeyote yule akiingia katika kiwanja cha ndani na kumwona mufalme bila kuitwa, huyo anapaswa kuuawa. Anayeweza kuponyoka ni yule tu ambaye mufalme atamunyooshea fimbo yake ya zahabu kwa kumuponyesha. Na mimi sijaitwa na mufalme, yapata mwezi muzima sasa.”