Esther 4:16 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Nenda ukawakusanye pamoja Wayahudi wote waliopo mjini Susa. Fungeni, msile wala msinywe kwa siku tatu, usiku na mchana, kwa ajili yangu. Na mimi na watumwa wa kike wangu tutafanya vivyo hivyo. Kisha, nitamwendea mfalme, ingawa ni kinyume cha sheria. Kama ni kuuawa, na niuawe.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Nenda, wakusanye Wayahudi wote walio Shushani, nanyi mfunge kwa ajili yangu. Msile wala kunywa kwa siku tatu, usiku na mchana. Mimi na wajakazi wangu tutafunga kama mnavyofanya. Baada ya kufanyika hili, nitaenda kwa mfalme, hata ingawa ni kinyume cha sheria. Ikiwa ni kuangamia na niangamie.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Uende ukawakusanye Wayahudi wote waliopo hapa Shushani, mkafunge kwa ajili yangu; msile wala kunywa muda wa siku tatu, usiku wala mchana, nami na wajakazi wangu tutafunga vile vile; kisha nitaingia kwa mfalme, kinyume cha sheria; nami nikiangamia, na niangamie.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Nenda ukawakusanye pamoja Wayahudi wote waliopo mjini Susa. Fungeni, msile wala msinywe kwa siku tatu, usiku na mchana, kwa ajili yangu. Na mimi na watumwa wa kike wangu tutafanya vivyo hivyo. Kisha, nitamwendea mfalme, ingawa ni kinyume cha sheria. Kama ni kuuawa, na niuawe.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Nenda, kusanya pamoja Wayahudi wote walioko Shushani, fungeni kwa ajili yangu. Msile wala kunywa kwa siku tatu, usiku na mchana. Mimi na wajakazi wangu tutafunga kama mnavyofanya. Baada ya kufanyika hili, nitakwenda kwa mfalme, hata ingawa ni kinyume cha sheria. Ikiwa ni kuangamia na niangamie.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Nenda, kusanya pamoja Wayahudi wote walioko Shushani, nanyi mfunge kwa ajili yangu. Msile wala kunywa kwa siku tatu, usiku na mchana. Mimi na wajakazi wangu tutafunga kama mnavyofanya. Baada ya kufanyika hili, nitakwenda kwa mfalme, hata ingawa ni kinyume cha sheria. Ikiwa ni kuangamia na niangamie.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nenda, uwakusanye Wayuda wote wanaopatikana humu Susani! Kisha mfunge mfungo kwa ajili yangu mimi na kuniombea, msile, wala msinywe siku tatu usiku na mchana! Mimi nami nitafunga hivyo pamoja na vijana wangu wa kike, kisha nitaingia kwake mfalme, ingawa ni mwiko. Kama ni kuangamia, basi, na niangamie!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Uende ukawakusanye Wayahudi wote waliopo hapa Shushani, mkafunge kwa ajili yangu; msile wala kunywa muda wa siku tatu, usiku wala mchana, nami na wajakazi wangu tutafunga vile vile; kisha nitaingia kwa mfalme, kinyume cha sheria; nami nikiangamia, na niangamie.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Kwenda uwakusanye pamoja Wayuda wote wanaokuwa katika muji wa Susani. Mufunge, musikule wala musikunywe kwa siku tatu, usiku na muchana, kwa ajili yangu. Na mimi na wajakazi wangu tutafanya vile vile. Kisha, nitamwendea mufalme, ingawa ni kinyume cha sheria. Kama ni kuuawa, niuawe.”