Esther 4:3 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Katika kila mkoa, mara tu amri ya mfalme ilipotangazwa, msiba mkubwa uliwakumba Wayahudi. Walifunga, wakalia na kuomboleza; na wengi wao walilala katika majivu wakiwa wamevaa magunia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika kila jimbo ambapo amri na agizo la mfalme lilifika, kulikuwa na maombolezo makuu miongoni mwa Wayahudi pamoja na kufunga, kulia na kuomboleza. Watu wengi wakalala juu ya magunia na majivu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na katika kila jimbo, ambako amri ya mfalme na mbiu yake imewasili, palikuwako msiba mkuu kwa Wayahudi, na kufunga, na kulia, na kuomboleza; hata na wengi wakalala juu ya gunia na majivu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Katika kila mkoa, mara tu amri ya mfalme ilipotangazwa, msiba mkubwa uliwakumba Wayahudi. Walifunga, wakalia na kuomboleza; na wengi wao walilala katika majivu wakiwa wamevaa magunia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika kila jimbo ambapo amri na agizo la mfalme lilifika, kulikuwa na maombolezo makuu miongoni mwa Wayahudi pamoja na kufunga, kulia na kuomboleza. Watu wengi wakalala juu ya nguo za magunia na majivu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika kila jimbo ambapo amri na agizo la mfalme lilifika, kulikuwa na maombolezo makuu miongoni mwa Wayahudi pamoja na kufunga, kulia na kuomboleza. Watu wengi wakalala juu ya nguo za magunia na majivu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Katika kila jimbo moja mahali po pote lile neno la mfalme lilipotangazwa, masikitiko makubwa yakawapata Wayuda, wakafunga mifungo pamoja na kulia machozi na kuomboleza; wengi wakakjitandikia magunia na majivu ya kuyalalia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na katika kila jimbo, ambako amri ya mfalme na mbiu yake imewasili, palikuwako msiba mkuu kwa Wayahudi, na kufunga, na kulia, na kuomboleza; hata na wengi wakalala juu ya gunia na majivu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika kila jimbo, mara tu amri ya mufalme ilipotangazwa, kilio kikubwa kiliwapata Wayuda. Wakafunga, wakalia na kuomboleza; na wengi wao wakalala katika majivu wakiwa wamevaa magunia.