Esther 4:8 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alimpa pia nakala moja ya tangazo lililokuwa limetolewa mjini Susa kuhusu kuangamizwa kwa Wayahudi, akamwomba amchukulie Esta, amweleze hali ilivyo, na kumwambia aende kumsihi mfalme na kumwomba awahurumie Wayahudi, watu wake Esta.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akampa nakala ya andiko la amri kwa ajili ya maangamizi yao, lililokuwa limechapishwa huko Shushani, kumwonesha Esta na kumwelezea. Mordekai akamwambia towashi amshawishi Esta kwenda mbele ya mfalme kuomba rehema na kumsihi kwa ajili ya watu wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Pia akampa na nakili ya andiko la mbiu ya kuwaangamiza, iliyotangazwa Shushani, ili amwonyeshe Esta, na kumweleza; tena amwagize aingie kwa mfalme, kumsihi na kuwaombea watu wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alimpa pia nakala moja ya tangazo lililokuwa limetolewa mjini Susa kuhusu kuangamizwa kwa Wayahudi, akamwomba amchukulie Esta, amweleze hali ilivyo, na kumwambia aende kumsihi mfalme na kumwomba awahurumie Wayahudi, watu wake Esta.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akampa nakala ya andiko la amri kwa ajili ya maangamizi yao, lililokuwa limechapishwa huko Shushani, kumwonyesha Esta na kumwelezea. Mordekai akamwambia towashi amshawishi Esta kwenda mbele ya mfalme kuomba rehema na kumsihi kwa ajili ya watu wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akampa nakala ya andiko la amri kwa ajili ya maangamizi yao, lililokuwa limechapishwa huko Shushani, kumwonyesha Esta na kumwelezea. Mordekai akamwambia towashi amshawishi Esta kwenda mbele ya mfalme kuomba rehema na kumsihi kwa ajili ya watu wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akampa karatasi iliyoandikwa ile mbiu iliyotangazwa Susani ya kuwatowesha, amwonyeshe Esteri na kumsimulia yote, kisha amwagize kwenda kwa mfalme kumlalamikia na kuuombea ukoo wake kwake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Pia akampa na nakili ya andiko la mbiu ya kuwaangamiza, iliyotangazwa Shushani, ili amwonyeshe Esta, na kumweleza; tena amwagize aingie kwa mfalme, kumsihi na kuwaombea watu wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akamupa na barua moja ya tangazo lililokuwa limetolewa katika muji wa Susani juu ya kuangamizwa kwa Wayuda, akamwomba amupelekee Esteri na kumwelezea jinsi hali inavyokuwa, na kumwambia aende kumusihi mufalme na kumwomba awahurumie Wayuda, watu wa Esteri.