Esther 5:1 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku ya tatu ya mfungo wake, Esta alivalia mavazi yake ya kimalkia, akaenda akasimama katika ua wa ndani wa nyumba ya mfalme, kuelekea ukumbi wa mfalme. Mfalme alikuwamo ndani, amekaa katika kiti chake cha enzi, kuelekea mlango wa nyumba ya mfalme.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku ya tatu, Esta alivaa mavazi yake ya kimalkia, naye akasimama katika ua wa ndani wa jumba la mfalme, mbele ya ukumbi wa mfalme. Naye mfalme alikuwa ameketi kwenye kiti chake cha kifalme katika ukumbi, akielekea langoni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa siku ya tatu Esta alijivika mavazi yake ya kifalme, akasimama katika ua wa ndani wa nyumba ya mfalme, kuielekea nyumba ya mfalme; naye mfalme akaketi juu ya kiti chake cha enzi katika nyumba ya mfalme, kuuelekea mlango wa nyumba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku ya tatu ya mfungo wake, Esta alivalia mavazi yake ya kimalkia, akaenda akasimama katika ua wa ndani wa nyumba ya mfalme, kuelekea ukumbi wa mfalme. Mfalme alikuwamo ndani, amekaa katika kiti chake cha enzi, kuelekea mlango wa nyumba ya mfalme.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku ya tatu Esta alivaa mavazi yake ya kimalkia, naye akasimama katika ua wa ndani wa jumba la mfalme, mbele ya ukumbi wa mfalme. Naye mfalme alikuwa akiketi katika kiti chake cha kifalme katika ukumbi, akielekea langoni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku ya tatu, Esta alivaa mavazi yake ya kimalkia, naye akasimama katika ua wa ndani wa jumba la mfalme, mbele ya ukumbi wa mfalme. Naye mfalme alikuwa akiketi katika kiti chake cha kifalme katika ukumbi, akielekea langoni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa siku ya tatu, Esteri akavaa mavazi ya kifalme, akaja kusimama katika ua wa ndani wa nyumba ya mfalme. Naye mfalme alikuwa amekaa katika kiti chake cha kifalme nyumbani mwake mwa kifalme, akajielekeza kuutazama mlango wa hiyo nyumba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa siku ya tatu Esta alijivika mavazi yake ya kifalme, akasimama katika ua wa ndani wa nyumba ya mfalme, kuielekea nyumba ya mfalme; naye mfalme akaketi juu ya kiti chake cha enzi katika nyumba ya mfalme, kuuelekea mlango wa nyumba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha siku tatu ya kufunga kwake, Esteri akavaa nguo zake za kimalkia, akaenda kusimama katika kiwanja cha ndani cha nyumba ya mufalme, kuelekea chumba cha mufalme. Mufalme alikuwa mule ndani akiikaa katika kiti chake cha kifalme, kuelekea mulango wa nyumba ya mufalme.