Esther 5:12 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hamani akaendelea kujitapa, “Isitoshe malkia Esta hakumwalika mtu mwingine yeyote pamoja na mfalme isipokuwa mimi tu. Hata kesho pia, ametualika mimi na mfalme.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hamani akaongeza, “Si hayo tu. Mimi ndiye mtu pekee ambaye Malkia Esta amemwalika kumsindikiza mfalme kwenye karamu aliyomwandalia. Naye amenialika pamoja na mfalme kesho.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Zaidi ya hayo Hamani akasema, Naye malkia Esta hakumkaribisha mtu ye yote pamoja na mfalme katika karamu aliyoiandaa, ila mimi peke yangu; hata na kesho pia nimealikwa naye pamoja na mfalme.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hamani akaendelea kujitapa, “Isitoshe malkia Esta hakumwalika mtu mwingine yeyote pamoja na mfalme isipokuwa mimi tu. Hata kesho pia, ametualika mimi na mfalme.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hamani akaongeza, “Si hayo tu. Mimi ndiye mtu pekee ambaye Malkia Esta amemwalika kumsindikiza mfalme kwenye karamu aliyomwandalia. Naye amenialika pamoja na mfalme kesho.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hamani akaongeza, “Si hayo tu. Mimi ndiye mtu pekee ambaye Malkia Esta amemwalika kumsindikiza mfalme kwenye karamu aliyomwandalia. Naye amenialika pamoja na mfalme kesho.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Hamani akasema: Naye Esteri, mkewe mfalme, hakualika mwingine, aje na mfalme kula karamu, aliyoifanya, ila mimi peke yangu. Hata kesho mimi nimealikwa naye kuja na mfalme.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Zaidi ya hayo Hamani akasema, Naye malkia Esta hakumkaribisha mtu ye yote pamoja na mfalme katika karamu aliyoiandaa, ila mimi peke yangu; hata na kesho pia nimealikwa naye pamoja na mfalme.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hamani akaendelea kujitapa: “Vilevile malkia Esteri hakumwalika mutu mwingine yeyote pamoja na mufalme isipokuwa mimi tu. Hata kesho tena, ametualika mimi na mufalme.