Esther 5:14 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Zereshi, mkewe, na marafiki zake, wakamshauri hivi: “Kwa nini asitengenezewe mti wa kuulia, wenye urefu wa mita ishirini na mbili? Kesho asubuhi, unaweza kuzungumza na mfalme ili Mordekai auawe juu yake, kisha uende ukale karamu na mfalme kwa furaha.” Wazo hilo lilimfurahisha Hamani, naye akatengeneza mti wa kuulia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Zereshi mkewe na rafiki zake wote wakamwambia, “Tengeneza mahali pa kuangika watu kimo chake dhiraa hamsini, kisha kesho asubuhi mwombe mfalme Mordekai aangikwe juu yake. Ndipo uende na mfalme kwenye karamu kwa furaha.” Shauri hili lilimpendeza Hamani, naye akajenga mahali pa kuangika watu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Zereshi mkewe akamwambia, na rafiki zake wote, Na ufanyizwe mti wa mikono hamsini urefu wake, na kesho asubuhi useme na mfalme ili Mordekai atundikwe juu yake; ndipo utakapoingia kwa kicheko pamoja na mfalme karamuni. Basi neno likampendeza Hamani, akaufanyiza ule mti.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Zereshi, mkewe, na marafiki zake, wakamshauri hivi: “Kwa nini asitengenezewe mti wa kuulia, wenye urefu wa mita ishirini na mbili? Kesho asubuhi, unaweza kuzungumza na mfalme ili Mordekai auawe juu yake, kisha uende ukale karamu na mfalme kwa furaha.” Wazo hilo lilimfurahisha Hamani, naye akatengeneza mti wa kuulia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Zereshi mkewe na rafiki zake wote wakamwambia, “Tengeneza mahali pa kuangika watu kimo chake dhiraa hamsini, kisha kesho asubuhi mwombe mfalme Mordekai aangikwe juu yake. Ndipo uende na mfalme kwenye karamu kwa furaha.” Shauri hili lilimpendeza Hamani, naye akajenga mahali pa kuangika watu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Zereshi mkewe na rafiki zake wote wakamwambia, “Tengeneza mahali pa kuangika watu kimo chake dhiraa hamsini, kisha kesho asubuhi mwombe mfalme Mordekai aangikwe juu yake. Ndipo uende na mfalme kwenye karamu kwa furaha.” Shauri hili lilimpendeza Hamani, naye akajenga mahali pa kuangika watu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mkewe Zeresi na wapenzi wake wote walipomwambia: Na wasimike mti mrefu wa mikono hamsini! Kisha umwambie mfalme kesho, wamtundike Mordekai, upate kwenda pamoja na mfalme karamuni na kufurahi! Shauri hili likampendeza Hamani, akausimika ule mti.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Zereshi mkewe akamwambia, na rafiki zake wote, Na ufanyizwe mti wa mikono hamsini urefu wake, na kesho asubuhi useme na mfalme ili Mordekai atundikwe juu yake; ndipo utakapoingia kwa kicheko pamoja na mfalme karamuni. Basi neno likampendeza Hamani, akaufanyiza ule mti.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, muke wake Zeresi na warafiki zake wakamushauria hivi: “Kwa nini asitengenezewe muti wa kutundikia, wenye urefu wa metre makumi mbili na mbili? Kesho asubui, unaweza kuzungumuza na mufalme kusudi Mordekayi auawe juu yake, kisha uende ukule karamu na mufalme kwa furaha.” Wazo hilo lilimufurahisha Hamani, naye akatengeneza muti ule.