Esther 5:2 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme alipomwona malkia Esta amesimama uani, alipendezwa naye, akamnyoshea fimbo ya dhahabu aliyokuwa ameshika mkononi mwake. Esta akakaribia, akagusa ncha ya fimbo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alipomwona Malkia Esta amesimama uani alipendezwa naye, akamnyooshea fimbo ya utawala ya dhahabu iliyokuwa mkononi mwake. Kwa hiyo Esta alikaribia na kuigusa ncha ya fimbo ya mfalme.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa, mfalme alipomwona malkia Esta amesimama uani, yeye akapata kibali machoni pake; naye mfalme akamnyoshea Esta fimbo ya dhahabu aliyokuwa nayo mkononi. Basi Esta akakaribia, akaigusa ncha ya fimbo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme alipomwona malkia Esta amesimama uani, alipendezwa naye, akamnyoshea fimbo ya dhahabu aliyokuwa ameshika mkononi mwake. Esta akakaribia, akagusa ncha ya fimbo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alipomwona Malkia Esta amesimama uani alipendezwa naye, akamnyoshea fimbo ya utawala ya dhahabu ile iliyokuwa mkononi mwake. Kwa hiyo Esta alikaribia na kuigusa ncha ya fimbo ya mfalme.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alipomwona Malkia Esta amesimama uani alipendezwa naye, akamnyooshea fimbo ya utawala ya dhahabu ile iliyokuwa mkononi mwake. Kwa hiyo Esta alikaribia na kuigusa ncha ya fimbo ya mfalme.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa, mfalme alipomwona Esteri, mkewe mfalme, akisimama uani, akaona upendeleo mbele yake, mfalme akampungia Esteri kwa bakora yake ya dhahabu iliyokuwa mkononi mwake. Ndipo, Esteri alipokuja kuugusa upembe wa hiyo bakora.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa, mfalme alipomwona malkia Esta amesimama uani, yeye akapata kibali machoni pake; naye mfalme akamnyoshea Esta fimbo ya dhahabu aliyokuwa nayo mkononi. Basi Esta akakaribia, akaigusa ncha ya fimbo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme alipomwona malkia Esteri akisimama katika kiwanja, Esteri akapata kukubaliwa mbele yake, naye akamunyooshea fimbo ya zahabu aliyokuwa akishika katika mukono wake. Esteri akakaribia, akagusa incha ya fimbo.