Esther 5:9 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hamani alitoka huko karamuni mwenye furaha tele na moyo mkunjufu. Lakini alipomwona Mordekai penye lango la ikulu, hasimami wala hampi heshima, Hamani akawaka hasira.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hamani alitoka siku hiyo kwa furaha na moyo mchangamfu. Lakini alipomwona Mordekai langoni mwa mfalme na kuona kwamba hakusimama wala hakuonesha hofu mbele yake, alijawa na ghadhabu dhidi ya Mordekai.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Hamani alitoka siku ile kwa furaha na ukunjufu wa moyo; lakini Hamani alipomwona Mordekai mlangoni pa mfalme, ya kwamba hasimami wala kutetemeka mbele yake, alijaa ghadhabu juu ya Mordekai.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hamani alitoka huko karamuni mwenye furaha tele na moyo mkunjufu. Lakini alipomwona Mordekai penye lango la ikulu, hasimami wala hampi heshima, Hamani akawaka hasira.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hamani alitoka siku hiyo kwa furaha na moyo mchangamfu. Lakini alipomwona Mordekai langoni mwa mfalme na kuona kwamba hakusimama wala hakuonyesha hofu mbele yake, alijawa na ghadhabu dhidi ya Mordekai.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hamani alitoka siku hiyo kwa furaha na moyo mchangamfu. Lakini alipomwona Mordekai langoni mwa mfalme na kuona kwamba hakusimama wala hakuonyesha hofu mbele yake, alijawa na ghadhabu dhidi ya Mordekai.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hamani akatoka mwake siku hiyo kwa kufurahi na kuchangamka moyoni. Lakini Hamani alipomwona Mordekai langoni kwa mfalme, asiinuke, wala asimwondokee, ndipo, makali yenye moto yalipomjaa Hamani moyoni kwa ajili ya Mordekai,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Hamani alitoka siku ile kwa furaha na ukunjufu wa moyo; lakini Hamani alipomwona Mordekai mlangoni pa mfalme, ya kwamba hasimami wala kutetemeka mbele yake, alijaa ghadhabu juu ya Mordekai.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hamani akatoka kule kwenye karamu mwenye furaha tele na moyo mukunjufu. Lakini alipomwona Mordekayi kwenye mulango wa nyumba ya kifalme, hasimami wala hamupi heshima, Hamani akawaka hasira.