Esther 6:10 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo mfalme akamwambia Hamani, “Fanya haraka! Chukua mavazi hayo na farasi, ukamtunukie heshima hii Mordekai, Myahudi ambaye hukaa penye lango la ikulu. Usiache kumfanyia hata jambo moja kati ya hayo uliyoyataja.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme akamwamuru Hamani, “Nenda mara moja, chukua joho na farasi na ufanye kama vile ulivyopendekeza kwa Mordekai Myahudi, akaaye langoni mwa mfalme. Usipuuze kufanya kitu chochote ulichoshauri.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi mfalme akamwambia Hamani, Hima! Twaa mavazi na farasi kama ulivyosema, ukamfanyizie vivyo hivyo Mordekai, Myahudi, aketiye mlangoni pa mfalme; lisipungue neno lo lote katika yote uliyoyasema.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo mfalme akamwambia Hamani, “Fanya haraka! Chukua mavazi hayo na farasi, ukamtunukie heshima hii Mordekai, Myahudi ambaye hukaa penye lango la ikulu. Usiache kumfanyia hata jambo moja kati ya hayo uliyoyataja.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme akamwamuru Hamani, “Nenda mara moja, chukua joho na farasi na ufanye kama vile ulivyopendekeza kwa Mordekai Myahudi, akaaye langoni mwa mfalme. Usipuuze kufanya kitu cho chote ulichoshauri.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme akamwamuru Hamani, “Nenda mara moja, chukua joho na farasi na ufanye kama vile ulivyopendekeza kwa Mordekai Myahudi, akaaye langoni mwa mfalme. Usipuuze kufanya kitu chochote ulichoshauri.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mfalme alipomwambia Hamani: Nenda upesi sasa hivi kuichukua hiyo nguo na huyo farasi, kama ulivyosema, umfanyizie vivyo hivyo Myuda Mordekai akaaye langoni kwa mfalme! Lakini usisahau hata neno moja katika hayo, uliyoyasema!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi mfalme akamwambia Hamani, Hima! Twaa mavazi na farasi kama ulivyosema, ukamfanyizie vivyo hivyo Mordekai, Myahudi, aketiye mlangoni pa mfalme; lisipungue neno lo lote katika yote uliyoyasema.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hapo mufalme akamwambia Hamani: “Fanya haraka! Twaa nguo hizi na farasi, umupatie Mordekayi heshima hii, yule Muyuda ambaye anaikaa kwenye mulango wa nyumba ya kifalme. Usiache kumufanyia hata jambo moja kati ya hayo uliyoyataja.”