Esther 6:11 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Hamani akachukua mavazi hayo na kumvisha Mordekai, akamtembeza kwenye uwanja wa mji akiwa juu ya farasi wa mfalme, huku anatangaza: “Hivi ndivyo anavyotendewa mtu ambaye mfalme amependa kumpa heshima.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo Hamani akachukua joho na farasi. Akamvika Mordekai, na kumpandisha juu ya farasi, akamtembeza katika barabara za mji akitangaza mbele yake, “Hivi ndivyo anavyotendewa mtu ambaye mfalme anapenda kumheshimu!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Hamani alipoyatwaa mavazi na farasi, akamvika Mordekai yale mavazi, akamrakibisha juu ya farasi kuipitia njia kuu ya mjini, akapiga mbiu mbele yake, Hivyo ndivyo atakavyofanyiziwa mtu yule ambaye mfalme apenda kumheshimu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Hamani akachukua mavazi hayo na kumvisha Mordekai, akamtembeza kwenye uwanja wa mji akiwa juu ya farasi wa mfalme, huku anatangaza: “Hivi ndivyo anavyotendewa mtu ambaye mfalme amependa kumpa heshima.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo Hamani akachukua joho na farasi. Akamvika Mordekai, na kumpandisha juu ya farasi akamtembeza katika barabara za mji akitangaza mbele yake, “Hivi ndivyo anavyofanyiwa mtu ambaye mfalme anapenda kumheshimu!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo Hamani akachukua joho na farasi. Akamvika Mordekai, na kumpandisha juu ya farasi akamtembeza katika barabara za mji akitangaza mbele yake, “Hivi ndivyo anavyofanyiwa mtu ambaye mfalme anapenda kumheshimu!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, Hamani akaichukua hiyo nguo na huyo farasi, akamvika Mordekai, kisha akampandisha uwanjani mwa mji, akapiga mbiu mbele yake kwamba: Hivi ndivyo, mtu anavyofanyiziwa, mfalme akipendezwa naye, amheshimu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Hamani alipoyatwaa mavazi na farasi, akamvika Mordekai yale mavazi, akamrakibisha juu ya farasi kuipitia njia kuu ya mjini, akapiga mbiu mbele yake, Hivyo ndivyo atakavyofanyiziwa mtu yule ambaye mfalme apenda kumheshimu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Hamani akatwaa nguo zile na kumuvalisha Mordekayi, akamutembeza kwenye kiwanja cha muji akiwa juu ya farasi wa mufalme, naye akitangaza: “Hivi ndivyo anavyotendewa mutu ambaye mufalme amependa kumupa heshima.”