Esther 6:2 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ikaonekana ilivyoandikwa jinsi Mordekai alivyongamua njama ya kumwua mfalme iliyokuwa imefanywa na Bigthana na Tereshi, wawili kati ya matowashi wa mfalme waliokuwa walinzi wa vyumba vya mfalme.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ikaonekana imeandikwa humo kwamba Mordekai alikuwa amefichua jinsi Bigthana na Tereshi, waliokuwa maafisa wawili wa mfalme, walinzi wa lango walivyokuwa wamepanga hila ya kumuua Mfalme Ahasuero.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikaonekana kuwa imeandikwa ya kwamba Mordekai aliwachongea Bigthana na Tereshi, wasimamizi wawili wa mfalme, katika hao waliolinda mlango, waliotaka kumtia mikono mfalme Ahasuero.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ikaonekana ilivyoandikwa jinsi Mordekai alivyong'amua njama ya kumwua mfalme iliyokuwa imefanywa na Bigthana na Tereshi, wawili kati ya matowashi wa mfalme waliokuwa walinzi wa vyumba vya mfalme.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kitabu hicho kilikutwa na kumbukumbu kwamba Mordekai alikuwa amefichua jinsi Bigthana na Tereshi, waliokuwa maafisa wawili wa mfalme, walinzi wa lango walivyokuwa wamepanga hila ya kumwua Mfalme Ahusuero.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kitabu hicho kilikutwa na kumbukumbu kwamba Mordekai alikuwa amefichua jinsi Bigthana na Tereshi, waliokuwa maafisa wawili wa mfalme, walinzi wa lango walivyokuwa wamepanga hila ya kumuua Mfalme Ahasuero.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
zikaoneka zile habari zilizoandikwa za kwamba: Mordekai ameumbua watumishi wa nyumbani mwa mfalme, Bigitana na Teresi, waliokuwa walinda mlango, waliotafuta njia ya kumwua mfalme Ahaswerosi kwa mikono yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikaonekana kuwa imeandikwa ya kwamba Mordekai aliwachongea Bigthana na Tereshi, wasimamizi wawili wa mfalme, katika hao waliolinda mlango, waliotaka kumtia mikono mfalme Ahasuero.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ikaonekana jinsi ilivyoandikwa ikielezwa jinsi Mordekayi alivyopasha habari ya shauri la kumwua mufalme iliyokuwa imefanywa na Bigitani na Teresi, hao wawili kati ya matowashi wa mufalme waliokuwa walinzi wa vyumba vya mufalme.