Esther 6:3 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme akauliza, “Je, tumempa Mordekai heshima au tuzo gani kwa jambo hili?” Watumishi wake wakamjibu, “Hujafanya kitu kwa ajili yake.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme akauliza, “Je, ni heshima na shukrani gani Mordekai alipokea kwa ajili ya jambo hili?” Watumishi wake wakajibu, “Hakuna lolote alilotendewa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mfalme akasema, Je! Ni heshima gani au jaha gani Mordekai aliyofanyiziwa kwa ajili ya hayo? Watumwa wa mfalme waliomhudumu wakamwambia, Hakuna alilofanyiziwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme akauliza, “Je, tumempa Mordekai heshima au tuzo gani kwa jambo hili?” Watumishi wake wakamjibu, “Hujafanya kitu kwa ajili yake.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme akauliza, “Je, ni heshima na shukrani gani Mordekai alipokea kwa ajili ya jambo hili?” Watumishi wake wakajibu, “Hakuna lo lote alilofanyiwa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme akauliza, “Je, ni heshima na shukrani gani Mordekai alipokea kwa ajili ya jambo hili?” Watumishi wake wakajibu, “Hakuna lolote alilofanyiwa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfalme akauliza: Mordekai amepata tunzo gani au ukuu gani kwa tendo hilo? Vijana wa mfalme waliomtumikia wakajibu: Hakuna alichofanyiziwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mfalme akasema, Je! Ni heshima gani au jaha gani Mordekai aliyofanyiziwa kwa ajili ya hayo? Watumwa wa mfalme waliomhudumu wakamwambia, Hakuna alilofanyiziwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme akauliza: “Tumemupa Mordekayi heshima au sifa gani kwa jambo hili?” Watumishi wake wakamujibu: “Hajafanyiwa jambo lolote.”