Esther 6:9 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
na mmoja wa washauri wako wa kuheshimika, ee mfalme, amvishe mtu huyo mavazi hayo ya kifalme, na kumwongoza mtu huyo akiwa amepanda farasi wako mpaka kwenye uwanja wa mji, huku anatangaza: ‘Hivi ndivyo anavyotendewa mtu ambaye mfalme amependa kumpa heshima.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha joho na farasi vikabidhiwe kwa mmoja wa wakuu wa mfalme anayeheshimika sana. Nao wamvike mtu yule ambaye mfalme anapenda kumheshimu, na aongozwe akiwa juu ya farasi kupitia barabara za mji, wakitangaza mbele yake, ‘Hivi ndivyo anavyotendewa mtu ambaye mfalme apenda kumheshimu!’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na yale mavazi na yule farasi akabidhiwe mkononi mmojawapo wa maakida wa mfalme aliye mstahiki; ili makusudi amvike yule ambaye mfalme apenda kumheshimu, na kumrakibisha juu ya farasi kuipitia njia kuu ya mjini, na kupiga mbiu mbele yake, kusema, Hivyo ndivyo atakavyofanyiziwa mtu yule ambaye mfalme apenda kumheshimu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
na mmoja wa washauri wako wa kuheshimika, ee mfalme, amvishe mtu huyo mavazi hayo ya kifalme, na kumwongoza mtu huyo akiwa amepanda farasi wako mpaka kwenye uwanja wa mji, huku anatangaza: ‘Hivi ndivyo anavyotendewa mtu ambaye mfalme amependa kumpa heshima.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha joho na farasi vikabidhiwe kwa mmojawapo wa wakuu wa mfalme anayeheshimika sana. Nao wamvike mtu yule ambaye mfalme anapenda kumheshimu, na aongozwe akiwa juu ya farasi kupitia barabara za mji, wakitangaza mbele yake, ‘Hivi ndivyo anavyofanyiwa mtu ambaye mfalme apenda kumheshimu!’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha joho na farasi vikabidhiwe kwa mmojawapo wa wakuu wa mfalme anayeheshimika sana. Nao wamvike mtu yule ambaye mfalme anapenda kumheshimu, na aongozwe akiwa juu ya farasi kupitia barabara za mji, wakitangaza mbele yake, ‘Hivi ndivyo anavyofanyiwa mtu ambaye mfalme apenda kumheshimu!’ ”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha mkuu mmoja wa mfalme mwenye macheo apewe hiyo nguo na huyo farasi, wamvike huyo mtu, mfalme apendezwaye naye, amheshimu, kisha wampandishe huyo farasi uwanjani mwa mji na kupiga mbiu mbele yake kwamba: Hivi ndivyo, mtu anavyofanyiziwa, mfalme akipendezwa naye, amheshimu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na yale mavazi na yule farasi akabidhiwe mkononi mmojawapo wa maakida wa mfalme aliye mstahiki; ili makusudi amvike yule ambaye mfalme apenda kumheshimu, na kumrakibisha juu ya farasi kuipitia njia kuu ya mjini, na kupiga mbiu mbele yake, kusema, Hivyo ndivyo atakavyofanyiziwa mtu yule ambaye mfalme apenda kumheshimu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
na mumoja wa washauri wako wa kuheshimika ee mufalme amuvalishe mutu yule nguo hizo za kifalme, na kumwongoza mutu yule akiwa amepanda juu ya farasi wako mpaka kwenye kiwanja cha muji, naye akitangaza: ‘Hivi ndivyo anavyotendewa mutu ambaye mufalme amependa kumupa heshima.’ ”