Esther 7:9 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Harbona, mmoja wa wale matowashi waliomhudumia mfalme, akasema, “Hamani amethubutu hata kutengeneza mti wa kumwulia Mordekai ambaye aliyaokoa maisha yako, ewe mfalme. Mti huo, wenye urefu wa mita ishirini na mbili, bado uko huko nyumbani kwake.” Hapo mfalme akaamuru, “Mwulie Hamani papo hapo.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Harbona, mmoja wa matowashi waliomtumikia mfalme, akasema, “Mahali pa kuangika watu penye urefu wa dhiraa hamsini pako nyumbani mwa Hamani. Alikuwa amepatengeneza kwa ajili ya Mordekai, ambaye alizungumza ili kumsaidia mfalme.” Mfalme akasema, “Mwangikeni juu yake!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo aliposema Harbona, msimamizi-wa-nyumba mmojawapo wa wale waliohudhuria mbele ya mfalme, Tazama, basi, mti wa mikono hamsini urefu wake, Hamani aliomwekea tayari Mordekai, ambaye alinena vema kwa ajili ya mfalme, upo umesimamishwa nyumbani kwa Hamani. Mfalme akasema, Mtundikeni juu yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Harbona, mmoja wa wale matowashi waliomhudumia mfalme, akasema, “Hamani amethubutu hata kutengeneza mti wa kumwulia Mordekai ambaye aliyaokoa maisha yako, ewe mfalme. Mti huo, wenye urefu wa mita ishirini na mbili, bado uko huko nyumbani kwake.” Hapo mfalme akaamuru, “Mwulie Hamani papo hapo.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Harbona, mmoja wa matowashi wanaomtumikia mfalme, akasema, “Mahali pa kuangika watu penye urefu wa mita ishirini na mbili pako nyumbani mwa Hamani. Alikuwa amepatengeneza kwa ajili ya Mordekai, ambaye alizungumza ili kumsaidia mfalme.” Mfalme akasema, “Mwangikeni juu yake!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Harbona, mmoja wa matowashi wanaomtumikia mfalme, akasema, “Mahali pa kuangika watu penye urefu wa mita ishirini na mbili pako nyumbani mwa Hamani. Alikuwa amepatengeneza kwa ajili ya Mordekai, ambaye alizungumza ili kumsaidia mfalme.” Mfalme akasema, “Mwangikeni juu yake!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Harbona, mmoja wao watumishi wa nyumbani waliomtumikia mfalme, akasema: Tazameni, ule mti, Hamani aliomsimikia Mordekai aliyesema mema ya kumponya mfalme, ungaliko kwenye nyumba ya Hamani, ni ule mrefu wa mikono hamsini. Ndipo, mfalme aliposema: Haya! Mtundikeni mumo humo!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo aliposema Harbona, msimamizi-wa-nyumba mmojawapo wa wale waliohudhuria mbele ya mfalme, Tazama, basi, mti wa mikono hamsini urefu wake, Hamani aliomwekea tayari Mordekai, ambaye alinena vema kwa ajili ya mfalme, upo umesimamishwa nyumbani kwa Hamani. Mfalme akasema, Mtundikeni juu yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Harbona, mumoja wa wale matowashi waliomutumikia mufalme, akasema: “Hamani amesubutu hata kutengeneza muti wa kumutundikia Mordekayi ambaye aliyaokoa maisha yako, ewe mufalme. Muti huo, wenye urefu wa metre makumi mbili na mbili, bado uko kule katika nyumba yake.” Hapo mufalme akaamuru: “Mumutundike Hamani juu ya muti uleule.”