Esther 8:1 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku hiyohiyo, mfalme Ahasuero alimkabidhi malkia Esta mali yote ya Hamani, adui ya Wayahudi. Esta akamjulisha mfalme kwamba Mordekai ni jamaa yake. Basi, tangu wakati huo, Mordekai akaruhusiwa kumwona mfalme.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku ile ile Mfalme Ahasuero akampa Malkia Esta shamba la Hamani, adui wa Wayahudi. Naye Mordekai akaja mbele ya mfalme, kwa kuwa Esta alikuwa amesema jinsi anavyohusiana naye.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Siku ile mfalme Ahasuero alimpa malkia Esta nyumba yake Hamani, yule adui ya Wayahudi. Mordekai naye akahudhuria mbele ya mfalme; kwa maana Esta alikuwa amedhihirisha alivyomhusu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku hiyohiyo, mfalme Ahasuero alimkabidhi malkia Esta mali yote ya Hamani, adui ya Wayahudi. Esta akamjulisha mfalme kwamba Mordekai ni jamaa yake. Basi, tangu wakati huo, Mordekai akaruhusiwa kumwona mfalme.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku ile ile Mfalme Ahusuero akampa Malkia Esta shamba la Hamani, adui wa Wayahudi. Naye Mordekai akaja mbele ya mfalme, kwa kuwa Esta alikuwa amesema jinsi anavyohusiana naye.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku ile ile Mfalme Ahasuero akampa Malkia Esta shamba la Hamani, adui wa Wayahudi. Naye Mordekai akaja mbele ya mfalme, kwa kuwa Esta alikuwa amesema jinsi anavyohusiana naye.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku hiyo mfalme Ahaswerosi akampa Esteri, mkewe mfalme, nyumba ya Hamani, aliyekuwa mpingani wao Wayuda. Mordekai akaja kwa mfalme, kwani Esteri alimsimulia mfalme, udugu wao ulivyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Siku ile mfalme Ahasuero alimpa malkia Esta nyumba yake Hamani, yule adui ya Wayahudi. Mordekai naye akahudhuria mbele ya mfalme; kwa maana Esta alikuwa amedhihirisha alivyomhusu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku ileile, mufalme Ahasuero akamupatia malkia Esteri mali yote ya Hamani, adui ya Wayuda. Esteri akamujulisha mufalme kwamba Mordekayi ni ndugu yake. Basi, tangu wakati ule, Mordekayi akaruhusiwa kumwona mufalme.