Esther 8:10 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mordekai alikuwa ameandika nyaraka hizo kwa jina la mfalme Ahasuero, akazipiga mhuri kwa pete ya mfalme. Na waliozipeleka walikuwa matarishi waliopanda farasi wenye nguvu waendao kasi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mordekai aliandika nyaraka kwa jina la Mfalme Ahasuero, akazitia muhuri kwa pete ya mfalme na kuzipeleka kwa matarishi, ambao waliendesha farasi wepesi waliozalishwa maalum kwa ajili ya mfalme.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaandika kwa jina la mfalme Ahasuero, na kutia muhuri kwa pete ya mfalme, akazipeleka barua kwa matarishi, wamepanda farasi, wamepanda wanyama wepesi sana waliotumika kwa huduma ya mfalme, ndio waliozalishwa katika zizi la mfalme.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mordekai alikuwa ameandika nyaraka hizo kwa jina la mfalme Ahasuero, akazipiga mhuri kwa pete ya mfalme. Na waliozipeleka walikuwa matarishi waliopanda farasi wenye nguvu waendao kasi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mordekai aliandika nyaraka kwa jina la Mfalme Ahusuero, akazitia muhuri kwa pete ya mfalme na kuzipeleka kwa njia ya matarishi, ambao waliendesha farasi waendao kasi waliozalishwa maalum kwa ajili ya mfalme.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mordekai aliandika nyaraka kwa jina la Mfalme Ahasuero, akazitia muhuri kwa pete ya mfalme na kuzipeleka kwa njia ya matarishi, ambao waliendesha farasi waendao kasi waliozalishwa maalum kwa ajili ya mfalme.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye akaziandika hizo barua katika jina la mfalme Ahaswerosi, akazitia muhuri kwa ile pete ya mfalme yenye muhuri, kisha akawapa wapiga mbio waliopanda farasi, wazipeleke; nao hao farasi waliowapanda walikuwa wa wakuu, walizaliwa katika makundi yaliyochaguliwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaandika kwa jina la mfalme Ahasuero, na kutia muhuri kwa pete ya mfalme, akazipeleka barua kwa matarishi, wamepanda farasi, wamepanda wanyama wepesi sana waliotumika kwa huduma ya mfalme, ndio waliozalishwa katika zizi la mfalme.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mordekayi alikuwa ameandika barua hizo kwa jina la mufalme Ahasuero, akazipiga muhuri kwa pete ya mufalme. Na waliozipeleka walikuwa wajumbe waliopanda juu ya farasi wenye nguvu wanaokimbia mbio.