Esther 8:11 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa njia ya nyaraka hizi mfalme aliwaruhusu Wayahudi katika kila mji kukusanyika ili kuyalinda maisha yao. Walikuwa na ruhusa ya kuharibu, kuua bila huruma na kuangamiza kundi lolote la watu au mkoa, lenye kuwashambulia kwa silaha pamoja na wanawake na watoto wao, na kuziteka nyara mali zao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waraka wa mfalme uliwaruhusu Wayahudi katika kila mji kuwa na haki ya kukusanyika na kujilinda wenyewe; kuharibu, kuua na kuangamiza jeshi lolote, taifa lolote au jimbo lile litakalowashambulia wao, wake zao, watoto wao na kuteka mali ya adui zao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Katika barua hizo mfalme aliwaruhusu Wayahudi wakusanyike katika kila mji na kuzisimamia maisha zao, kuangamiza, na kuua, na kulifisha jeshi lote la watu na la jimbo watakaowaondokea, wao na wadogo wao na wanawake; na kuyachukua mali yao kuwa nyara;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa njia ya nyaraka hizi mfalme aliwaruhusu Wayahudi katika kila mji kukusanyika ili kuyalinda maisha yao. Walikuwa na ruhusa ya kuharibu, kuua bila huruma na kuangamiza kundi lolote la watu au mkoa, lenye kuwashambulia kwa silaha pamoja na wanawake na watoto wao, na kuziteka nyara mali zao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Waraka wa mfalme uliwaruhusu Wayahudi katika kila mji kuwa na haki ya kukusanyika na kujilinda wenyewe; kuharibu, kuua na kuangamiza jeshi lo lote, taifa lo lote au jimbo lile litakalowashambulia wao, wake zao, watoto wao na kuteka mali za adui zao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waraka wa mfalme uliwaruhusu Wayahudi katika kila mji kuwa na haki ya kukusanyika na kujilinda wenyewe; kuharibu, kuua na kuangamiza jeshi lolote, taifa lolote au jimbo lile litakalowashambulia wao, wake zao, watoto wao na kuteka mali za adui zao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yaliyoandikwa ni haya: Mfalme amewapa ruhusa Wayuda waliomo katika miji yote, wakusanyike katika kila mji mmoja kujisimamia wenyewe na kujiokoa, wakiwatowesha kwa kuwaua na kwa kuwaangamiza vikosi vyote vya watu wa kila kabila na wa kila jimbo watakaowashambulia, hata watoto na wanawake, kisha waziteke nazo mali zao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Katika barua hizo mfalme aliwaruhusu Wayahudi wakusanyike katika kila mji na kuzisimamia maisha zao, kuangamiza, na kuua, na kulifisha jeshi lote la watu na la jimbo watakaowaondokea, wao na wadogo wao na wanawake; na kuyachukua mali yao kuwa nyara;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa njia ya barua hizi mufalme akawaruhusu Wayuda katika kila muji kukusanyika kwa kuyalinda maisha yao. Walikuwa na ruhusa ya kuharibu, kuua bila huruma na kuangamiza kundi lolote la watu au jimbo, lenye kuwashambulia kwa silaha pamoja na wanawake na watoto wao, na kunyanganya mali zao.