Esther 8:15 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mordekai alipotoka ikulu kwa mfalme, akiwa amevalia mavazi ya kifalme ya rangi ya urujuani na nyeupe, joho la kitani safi la rangi ya zambarau, na taji kubwa ya dhahabu, mji wa Susa ulijaa shangwe na vigelegele.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mordekai akaondoka mbele ya mfalme akiwa amevaa mavazi ya kifalme ya buluu na nyeupe, taji kubwa la dhahabu na joho la zambarau la kitani safi. Na mji wa Shushani ukasherehekea kwa furaha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Mordekai akatoka usoni pa mfalme, amevaa mavazi ya kifalme, ya rangi ya samawi na nyeupe, mwenye taji kubwa ya dhahabu, na joho ya kitani safi na rangi ya zambarau. Mji wa Shushani wakapaza sauti, wakashangilia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mordekai alipotoka ikulu kwa mfalme, akiwa amevalia mavazi ya kifalme ya rangi ya urujuani na nyeupe, joho la kitani safi la rangi ya zambarau, na taji kubwa ya dhahabu, mji wa Susa ulijaa shangwe na vigelegele.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mordekai akaondoka mbele ya mfalme akiwa amevaa mavazi ya kifalme ya buluu na nyeupe, taji kubwa la dhahabu na joho la zambarau la kitani safi. Na mji wa Shushani ukasherekea kwa furaha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mordekai akaondoka mbele ya mfalme akiwa amevaa mavazi ya kifalme ya buluu na nyeupe, taji kubwa la dhahabu na joho la zambarau la kitani safi. Na mji wa Shushani ukasherehekea kwa furaha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Mordekai akatoka usoni pa mfalme, akawa amevaa vazi la kifalme la nguo ya kifalme nyeusinyeusi na nyeupe, napo kichwani amevaa kilemba kikubwa cha kifalme cha dhahabu, tena amevaa joho la bafta lenye nguo nyekundu za kifalme. Nao mji wa Susani ukajaa vigelegele na mashangilio.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Mordekai akatoka usoni pa mfalme, amevaa mavazi ya kifalme, ya rangi ya samawi na nyeupe, mwenye taji kubwa ya dhahabu, na joho ya kitani safi na rangi ya zambarau. Mji wa Shushani wakapaza sauti, wakashangilia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mordekayi alipotoka katika nyumba kwa mufalme, akiwa amevaa nguo ya kifalme ya rangi ya mayungiyungi na nyeupe, koti la kitani safi la rangi nyekundu, na taji kubwa ya zahabu, muji wa Susani ukajaa shangwe na vigelegele.