Esther 8:17 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Katika kila mkoa na kila mji, popote pale tangazo hili liliposomwa, Wayahudi walifurahi na kushangilia, wakafanya sherehe na mapumziko; na watu wengine wengi wakajifanya kuwa Wayahudi, maana waliwaogopa sana Wayahudi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika kila jimbo na katika kila jiji, popote waraka wa mfalme ulipofika, kulikuwa na furaha na shangwe miongoni mwa Wayahudi, pamoja na karamu na kushangilia. Na watu wengi wa mataifa mengine wakajifanya Wayahudi kwa sababu ya kuwahofu Wayahudi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na katika kila jimbo, na kila mji, po pote palipowasili amri ya mfalme na mbiu yake, Wayahudi wakapata furaha na shangwe, karamu na sikukuu. Hata wengi wa watu wa nchi wakajifanya Wayahudi, kwa kuwa hofu ya Wayahudi imewaangukia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Katika kila mkoa na kila mji, popote pale tangazo hili liliposomwa, Wayahudi walifurahi na kushangilia, wakafanya sherehe na mapumziko; na watu wengine wengi wakajifanya kuwa Wayahudi, maana waliwaogopa sana Wayahudi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika kila jimbo na katika kila jiji, popote waraka wa mfalme ulipofika, kulikuwepo furaha na shangwe miongoni mwa Wayahudi, pamoja na karamu na kushangilia. Na watu wengi wa mataifa mengine wakajifanya Wayahudi kwa sababu ya kuwahofu Wayahudi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika kila jimbo na katika kila jiji, popote waraka wa mfalme ulipofika, kulikuwepo furaha na shangwe miongoni mwa Wayahudi, pamoja na karamu na kushangilia. Na watu wengi wa mataifa mengine wakajifanya Wayahudi kwa sababu ya kuwahofu Wayahudi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Katika kila jimbo na katika kila mji mmoja mahali po pote, lile neno la mfalme lilipotangazwa, pakawa na furaha na macheko kwa Wayuda, hata karamu na sikukuu, nao watu wengi wa hizo nchi wakajigeuza kuwa Wayuda, kwa kuguiwa na woga wa kuwaogopa Wayuda.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na katika kila jimbo, na kila mji, po pote palipowasili amri ya mfalme na mbiu yake, Wayahudi wakapata furaha na shangwe, karamu na sikukuu. Hata wengi wa watu wa nchi wakajifanya Wayahudi, kwa kuwa hofu ya Wayahudi imewaangukia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika kila jimbo na kila muji, popote pale tangazo hili liliposomwa, Wayuda wakafurahi na kushangilia, wakafanya sherehe na mapumziko; na watu wengine wengi wakajifanya kuwa Wayuda, maana waliwaogopa sana Wayuda.