Esther 8:2 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme akaivua pete yake ya mhuri aliyokuwa amemnyanganya Hamani, akampa Mordekai. Esta naye akampa Mordekai mamlaka juu ya mali ya Hamani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme akaivua pete yake ya muhuri, ambayo alikuwa amemnyang’anya Hamani, akampa Mordekai, naye Esta akamweka Mordekai asimamie shamba la Hamani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi mfalme akaivua pete yake, aliyompokonya Hamani, akampa Mordekai. Naye Esta akamweka Mordekai kuwa juu ya mlango wake Hamani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme akaivua pete yake ya mhuri aliyokuwa amemnyang'anya Hamani, akampa Mordekai. Esta naye akampa Mordekai mamlaka juu ya mali ya Hamani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme akaivua pete yake ya muhuri, ambayo alikuwa amemnyang'anya Hamani, akampa Mordekai naye Esta akamweka Mordekai juu ya shamba la Hamani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme akaivua pete yake ya muhuri, ambayo alikuwa amemnyang’anya Hamani, akampa Mordekai, naye Esta akamweka Mordekai juu ya shamba la Hamani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mfalme alipoondoa kidoleni pete yake yenye muhuri, aliyomvua Hamani, akampa Mordekai. Naye Esteri akamkalisha Mordekai katika nyumba ya Hamani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi mfalme akaivua pete yake, aliyompokonya Hamani, akampa Mordekai. Naye Esta akamweka Mordekai kuwa juu ya mlango wake Hamani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme akaivua pete yake ya muhuri aliyokuwa amemunyanganya Hamani, akamupa Mordekayi. Esteri naye akamupa Mordekayi mamlaka juu ya mali ya Hamani.