Esther 8:5 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Ukipenda, ewe mfalme, na kama unanijali na ukiona inafaa, tafadhali, toa tangazo la kufutilia mbali mipango ambayo Hamani alikuwa ameamuru itekelezwe. Mipango hiyo ni ile ya mwana wa Hamedatha, mzaliwa wa Agagi, aliyopanga ili kuwaangamiza Wayahudi wote katika mikoa yote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Esta akasema, “Ikimpendeza mfalme, nami nikipata kibali, naye akiona ni jambo lililo sawa kunitendea, na akipendezwa nami, basi iandikwe amri ya kuzitangua barua zile Hamani mwana wa Hamedatha Mwagagi, alizotunga na kuandika kuangamiza Wayahudi katika majimbo yote ya mfalme.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasema, Mfalme akiona vema, nami nikiwa nimepata kibali machoni pake, na neno likionekana jema mbele ya mfalme, nami nikimpendeza machoni pake, iandikwe kuzitangua barua za Hamani bin Hamedatha, Mwagagi, alizotunga na kuziandika ili kuwaangamiza Wayahudi walioko katika majimbo yote ya mfalme.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Ukipenda, ewe mfalme, na kama unanijali na ukiona inafaa, tafadhali, toa tangazo la kufutilia mbali mipango ambayo Hamani alikuwa ameamuru itekelezwe. Mipango hiyo ni ile ya mwana wa Hamedatha, mzaliwa wa Agagi, aliyopanga ili kuwaangamiza Wayahudi wote katika mikoa yote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Esta akasema, “Kama ikimpendeza mfalme, nami kama nikipata kibali naye akiona ni jambo lililo sawa kunitendea na kama akipendezwa nami, basi iandikwe amri ya kuzitangua barua zile Hamani mwana wa Hamedatha, Mwagagi, alizotunga na kuandika kuangamiza Wayahudi katika majimbo yote ya mfalme.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Esta akasema, “Kama ikimpendeza mfalme, nami kama nikipata kibali naye akiona ni jambo lililo sawa kunitendea na kama akipendezwa nami, basi iandikwe amri ya kuzitangua barua zile Hamani mwana wa Hamedatha, Mwagagi, alizotunga na kuandika kuangamiza Wayahudi katika majimbo yote ya mfalme.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akasema: Vikiwa vema kwake mfalme, nami nikiwa nimeona upendeleo mbele yake, nalo neno hili likifaa mbele yake mfalme, mimi nikiwa mwema machoni pake, basi, na ziandikwe barua za kuzitangua zile barua zenya lile shauri baya la Hamani, mwana wa Hamedata wa Agagi, alizoziandika za kuwaangamiza Wayuda wote walioko katika majimbo yote ya mfalme.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasema, Mfalme akiona vema, nami nikiwa nimepata kibali machoni pake, na neno likionekana jema mbele ya mfalme, nami nikimpendeza machoni pake, iandikwe kuzitangua barua za Hamani bin Hamedatha, Mwagagi, alizotunga na kuziandika ili kuwaangamiza Wayahudi walioko katika majimbo yote ya mfalme.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Ikikupendeza, ewe mufalme, na kama nimepata kukubaliwa mbele yako, ukiona ni vizuri nami nikikupendeza, tafazali, toa tangazo la kuvunja mipango ambayo Hamani alikuwa ameamuru itimizwe. Mipango hiyo ni ile ya mwana wa Hamedata, wa uzao wa Agagi, aliyopanga kwa kuwaangamiza Wayuda wote katika majimbo yote.