Esther 8:9 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, mnamo siku ya ishirini na tatu ya mwezi wa tatu uitwao Siwani, Mordekai aliwaita makatibu wote wa mfalme, akawaagiza waandike barua kwa Wayahudi na wakuu, watawala na maofisa wa mikoa yote 127, kuanzia India mpaka Kushi. Nyaraka hizo ziliandikwa kwa kila mkoa katika lugha yake na hati yake ya maandishi, hali kadhalika kwa Wayahudi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mara moja waandishi wa mfalme wakaitwa kwenye siku ya ishirini na tatu, mwezi wa tatu, ndio mwezi wa Siwani. Wakaandika yote Mordekai aliyoamuru kwa Wayahudi, kwa majemadari, watawala na wakuu wa majimbo mia moja na ishirini na saba (127) kuanzia Bara Hindi hadi Kushi. Maagizo haya yaliandikwa kwa maandishi ya kila jimbo na kwa lugha ya kila mtu pia kwa Wayahudi kwa maandishi yao wenyewe na lugha yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, waandishi wa mfalme wakaitwa pale pale, siku ya ishirini na tatu ya mwezi wa tatu, ndio mwezi wa Siwani; na kama vile Mordekai alivyoamuru, Wayahudi wakaandikiwa, pamoja na maakida na maliwali, na wakuu wa majimbo toka Bara Hindi mpaka Kushi, majimbo mia na ishirini na saba, kila jimbo kwa mwandiko wake, na kila taifa kwa lugha yake; na Wayahudi kwa mwandiko wao na kwa lugha yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, mnamo siku ya ishirini na tatu ya mwezi wa tatu uitwao Siwani, Mordekai aliwaita makatibu wote wa mfalme, akawaagiza waandike barua kwa Wayahudi na wakuu, watawala na maofisa wa mikoa yote 127, kuanzia India mpaka Kushi. Nyaraka hizo ziliandikwa kwa kila mkoa katika lugha yake na hati yake ya maandishi, hali kadhalika kwa Wayahudi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mara moja waandishi wa mfalme wakaitwa kwenye siku ya ishirini na tatu, mwezi wa tatu, ndio mwezi wa Siwani. Wakaandika yote Mordekai aliyoamuru kwa Wayahudi, kwa majemadari, watawala na wakuu wa majimbo 127 kuanzia Bara Hindi mpaka Kushi. Maagizo haya yaliandikwa kwa maandishi ya kila jimbo na kwa lugha ya kila mtu pia kwa Wayahudi kwa maandishi yao wenyewe na lugha yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mara moja waandishi wa mfalme wakaitwa kwenye siku ya ishirini na tatu, mwezi wa tatu, ndio mwezi wa Siwani. Wakaandika yote Mordekai aliyoamuru kwa Wayahudi, kwa majemadari, watawala na wakuu wa majimbo 127 kuanzia Bara Hindi mpaka Kushi. Maagizo haya yaliandikwa kwa maandishi ya kila jimbo na kwa lugha ya kila mtu pia kwa Wayahudi kwa maandishi yao wenyewe na lugha yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakaitwa waandishi wa mfalme wakati huo wa mwezi wa tatu, ndio mwezi wa Siwani, siku ya ishirini na tatu, yote Mordekai aliyoyaagiza yakaandikwa baruani kwa Wayuda na kwa wenye amri na kwa watawala nchi na kwa wakuu wa majimbo kuanzia nchi ya Uhindi kuifikisha hata nchi ya Nubi, majimbo yote ni 127; yakaandikwa kwa kila jimbo katika maandiko ya kwao na kwa kila kabila katika msemo wa kwao, hata kwa Wayuda katika maandiko ya kwao na katika msemo wa kwao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, waandishi wa mfalme wakaitwa pale pale, siku ya ishirini na tatu ya mwezi wa tatu, ndio mwezi wa Siwani; na kama vile Mordekai alivyoamuru, Wayahudi wakaandikiwa, pamoja na maakida na maliwali, na wakuu wa majimbo toka Bara Hindi mpaka Kushi, majimbo mia na ishirini na saba, kila jimbo kwa mwandiko wake, na kila taifa kwa lugha yake; na Wayahudi kwa mwandiko wao na kwa lugha yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, katika siku ya makumi mbili na tatu ya mwezi wa tatu inayoitwa Siwani, Mordekayi akawaita waandishi wote wa mufalme, akawaagiza waandike barua kwa Wayuda na wakubwa, watawala na wakubwa wa majimbo yote mia moja makumi mbili na saba, kuanzia Uhindi mpaka Etiopia. Barua hizo zikaandikwa kwa kila jimbo katika luga yake na sawasawa na maandiko yake, vilevile na kwa Wayuda kwa maandiko yao na luga yao.