Esther 9:1 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili, yaani mwezi wa Adari, ilipofika, siku ambayo tangazo la mfalme lingetekelezwa, na maadui wa Wayahudi walitarajia kuwashinda Wayahudi, iligeuzwa kuwa siku ya ushindi kwa Wayahudi dhidi ya adui zao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili, yaani mwezi wa Adari, amri iliyoagizwa na mfalme ilikuwa itekelezwe. Siku hii adui wa Wayahudi walikuwa wametumaini kuwashinda, lakini sasa mambo yaliwageukia na Wayahudi wakawashinda wale waliokuwa wanawachukia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata ulipofika mwezi wa kumi na mbili, ndio mwezi wa Adari, siku yake ya kumi na tatu, amri ya mfalme na mbiu yake ilipowadia kutekelezwa; ambayo siku ile adui za Wayahudi walitumaini kuwatawala, bali kumebadilika kinyume, hata Wayahudi waliwatawala wale waliowachukia;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili, yaani mwezi wa Adari, ilipofika, siku ambayo tangazo la mfalme lingetekelezwa, na maadui wa Wayahudi walitarajia kuwashinda Wayahudi, iligeuzwa kuwa siku ya ushindi kwa Wayahudi dhidi ya adui zao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili, yaani mwezi wa Adari, amri iliyoagizwa na mfalme ilikuwa itekelezwe. Siku hii adui wa Wayahudi walikuwa wametumaini kuwashinda, lakini sasa mambo yaliwageukia na Wayahudi wakawashinda wale waliokuwa wanawachukia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili, yaani mwezi wa Adari, amri iliyoagizwa na mfalme ilikuwa itekelezwe. Siku hii adui wa Wayahudi walikuwa wametumaini kuwashinda, lakini sasa mambo yaliwageukia na Wayahudi wakawashinda wale waliokuwa wanawachukia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Katika mwezi wa kumi na mbili, ndio mwezi wa Adari, siku ya kumi na tatu ilikuwa ile siku iliyotangazwa kwamba: Lile neno la mfalme, aliloliagiza, lifanyike siku hiyo; ndipo, adui za Wayuda walipongojea kuwashinda, lakini ikageuzwa, Wayuda wakapata wao kuwashinda wachukivu wao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata ulipofika mwezi wa kumi na mbili, ndio mwezi wa Adari, siku yake ya kumi na tatu, amri ya mfalme na mbiu yake ilipowadia kutekelezwa; ambayo siku ile adui za Wayahudi walitumaini kuwatawala, bali kumebadilika kinyume, hata Wayahudi waliwatawala wale waliowachukia;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili, ni kusema mwezi wa Adari, ilipofika, siku ambayo tangazo la mufalme lingetimizwa, na waadui za Wayuda walitarajia kuwashinda Wayuda, ikageuzwa kuwa siku ya ushindi kwa Wayuda juu ya waadui zao.