Esther 9:11 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku hiyohiyo, mfalme alijulishwa idadi ya watu waliouawa katika mji mkuu wa Susa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme aliarifiwa siku hiyo hiyo hesabu ya waliouawa katika ngome ya Shushani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Siku ile mfalme akaletewa hesabu ya hao waliouawa huko Shushani ngomeni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku hiyohiyo, mfalme alijulishwa idadi ya watu waliouawa katika mji mkuu wa Susa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme aliarifiwa siku iyo hiyo hesabu ya waliouawa katika ngome ya Shushani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme aliarifiwa siku iyo hiyo hesabu ya waliouawa katika ngome ya Shushani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku hiyo mfalme alipopata hesabu yao waliouawa Susani, mlimokuwa na jumba la mfalme,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Siku ile mfalme akaletewa hesabu ya hao waliouawa huko Shushani ngomeni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku ileile, mufalme akajulishwa jumla ya watu waliouawa katika muji mukubwa wa Susani.