Esther 9:12 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo mfalme akamwambia malkia Esta: “Katika mji mkuu peke yake Wayahudi wamewaua watu 500, pamoja na wana kumi wa Hamani. Unafikiri wamefanyaje huko mikoani! Unataka nini sasa? Maana utatimiziwa. Niambie, unataka nini zaidi, nawe utapewa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme akamwambia Malkia Esta, “Wayahudi wamewaua wanaume mia tano, na wana kumi wa Hamani ndani ya ngome ya Shushani. Wamefanyaje katika majimbo mengine ya mfalme yaliyobaki? Je, sasa haja yako ni nini? Nayo pia utapewa. Nalo ombi lako ni nini? Nalo utatendewa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mfalme akamwambia malkia Esta, Wayahudi wamewaua watu mia tano hapa Shushani ngomeni na kuwaangamiza, pamoja na wana kumi wa Hamani, je! Wamefanyaje basi katika majimbo ya mfalme yaliyosalia! Basi, una nini uombalo? Nawe utapewa; ama unayo haja gani tena? Nayo itatimizwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo mfalme akamwambia malkia Esta: “Katika mji mkuu peke yake Wayahudi wamewaua watu 500, pamoja na wana kumi wa Hamani. Unafikiri wamefanyaje huko mikoani! Unataka nini sasa? Maana utatimiziwa. Niambie, unataka nini zaidi, nawe utapewa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme akamwambia Malkia Esta, “Wayahudi wamewaua wanaume 500 na wana kumi wa Hamani ndani ya ngome ya Shushani. Wamefanyaje katika majimbo mengine ya mfalme yaliyobaki? Je, sasa haja yako ni nini? Nayo pia utapewa. Nalo ombi lako ni nini? Nalo utafanyiwa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme akamwambia Malkia Esta, “Wayahudi wamewaua wanaume 500 na wana kumi wa Hamani ndani ya ngome ya Shushani. Wamefanyaje katika majimbo mengine ya mfalme yaliyobaki? Je, sasa haja yako ni nini? Nayo pia utapewa. Nalo ombi lako ni nini? Nalo utafanyiwa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
mfalme akamwambia Esteri, mkewe mfalme: Humu susani, mlimo na jumba la mfalme, Wayuda wameua na kuwaangamiza watu 500 na wana kumi wa Hamani; sijui, waliyoyafanya katika majimbo mengine ya mfalme yaliyosalia. Lakini unayoyaomba utapewa; nayo unayoyataka yatafanyika tena.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mfalme akamwambia malkia Esta, Wayahudi wamewaua watu mia tano hapa Shushani ngomeni na kuwaangamiza, pamoja na wana kumi wa Hamani, je! Wamefanyaje basi katika majimbo ya mfalme yaliyosalia! Basi, una nini uombalo? Nawe utapewa; ama unayo haja gani tena? Nayo itatimizwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu mufalme akamwambia malkia Esteri: “Katika muji mukubwa peke yake Wayuda wamewaua watu mia tano, pamoja na wana kumi wa Hamani. Unafikiri wamefanya nini kule katika majimbo! Unataka nini sasa? Maana utatimiziwa. Uniambie, unataka nini zaidi, nawe utapewa.”