Esther 9:13 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Esta akasema, “Ukiona ni vema, ewe mfalme, kesho waruhusu Wayahudi waliomo Susa wafanye kama agizo la leo lilivyokuwa. Tena, uamuru wana kumi wa Hamani watundikwe kwenye miti ya kuulia.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Esta akajibu, “Ikimpendeza mfalme, uwape ruhusa Wayahudi walio Shushani warudie amri ya leo kesho pia, na wana wa Hamani kumi wanyongwe mahali pa kunyongea watu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Esta aliposema, Mfalme akiona vema, Wayahudi walioko Shushani na wapewe ruhusa kufanya tena kesho sawasawa na mbiu ya leo, na hao wana kumi wa Hamani watundikwe juu ya mti ule.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Esta akasema, “Ukiona ni vema, ewe mfalme, kesho waruhusu Wayahudi waliomo Susa wafanye kama agizo la leo lilivyokuwa. Tena, uamuru wana kumi wa Hamani watundikwe kwenye miti ya kuulia.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Esta akajibu, “Ikimpendeza mfalme, uwape ruhusa Wayahudi walioko Shushani warudie amri ya leo kesho pia, na wana wa Hamani kumi wanyongwe mahali pa kunyongea watu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Esta akajibu, “Ikimpendeza mfalme, uwape ruhusa Wayahudi walioko Shushani warudie amri ya leo kesho pia, na wana wa Hamani kumi wanyongwe mahali pa kunyongea watu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Esteri akasema: Vikiwa vema kwake mfalme, Wayuda waliomo Susani wapewe ruhusa hata kesho kufanya, kama walivyofanya leo, nao wale wana kumi wa Hamani wawatundike katika ule mti.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Esta aliposema, Mfalme akiona vema, Wayahudi walioko Shushani na wapewe ruhusa kufanya tena kesho sawasawa na mbiu ya leo, na hao wana kumi wa Hamani watundikwe juu ya mti ule.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Esteri akasema: “Ikikupendeza, ewe mufalme, kesho uwaruhusu Wayuda wanaokuwa Susani wafanye kama agizo la leo lilivyokuwa. Tena, uamuru wana kumi wa Hamani watundikwe kwenye miti.”