Esther 9:16 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wayahudi waliokuwa katika mikoa nao pia walijiandaa kuyalinda maisha yao. Wakaokolewa kutoka kwa maadui wao; waliwaua watu wapatao 75,000, lakini hawakuchukua nyara.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati ule ule, Wayahudi wengine waliokuwa kwenye majimbo ya mfalme, wakakusanyika kujilinda nao wakapata nafuu kutokana na adui zao. Waliua adui zao wapatao elfu sabini na tano, lakini hawakugusa nyara zao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao Wayahudi wengine waliokaa katika majimbo ya mfalme walikusanyika, wakazishindania maisha zao, wakajipatia raha mbele ya adui zao, wakawaua waliowachukia, watu sabini na tano elfu; walakini juu ya nyara hawakuweka mikono.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wayahudi waliokuwa katika mikoa nao pia walijiandaa kuyalinda maisha yao. Wakaokolewa kutoka kwa maadui wao; waliwaua watu wapatao 75,000, lakini hawakuchukua nyara.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati ule ule, Wayahudi wengine waliokuwa kwenye majimbo ya mfalme, wakakusanyika kujilinda nao wakapata nafuu kutokana na adui zao. Waliua adui zao wapatao 75,000 lakini hawakugusa nyara zao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati ule ule, Wayahudi wengine waliokuwa kwenye majimbo ya mfalme, wakakusanyika kujilinda nao wakapata nafuu kutokana na adui zao. Waliua adui zao wapatao 75,000 lakini hawakugusa nyara zao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao wale Wayuda wengine waliokuwa katika majimbo wakakusanyika, wajisimamie wenyewe na kujiokoa, wajipatie utulivu kwao adui zao, wakaua wachukivu wao 75000, lakini mali zao hawakuziteka kwa mikono yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao Wayahudi wengine waliokaa katika majimbo ya mfalme walikusanyika, wakazishindania maisha zao, wakajipatia raha mbele ya adui zao, wakawaua waliowachukia, watu sabini na tano elfu; walakini juu ya nyara hawakuweka mikono.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wayuda waliokuwa katika majimbo nao vilevile wakajitayarisha kuyalinda maisha yao. Wakaokolewa kutoka kwa waadui zao, wakawaua watu yapata elfu kumi na tano, lakini hawakunyanganya mali zao.