Esther 9:19 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kutokana na sababu hii, Wayahudi wakaao vijijini na katika miji midogo huadhimisha siku ya kumi na nne ya mwezi wa Adari kuwa sikukuu ya furaha, na kupelekeana zawadi hali wale waishio katika miji mikubwa huadhimisha siku ya kumi na tano ya mwezi wa Adari kama siku ya mapumziko, wakapelekeana pia zawadi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndiyo sababu Wayahudi wanaokaa vijijini na katika miji midogo huadhimisha siku ya kumi na nne ya mwezi wa Adari kama siku ya furaha na karamu, siku ambayo wao hupeana zawadi mmoja kwa mwingine.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu hii Wayahudi wa vijijini, wakaao katika miji isiyo na boma, huishika siku ya kumi na nne ya mwezi wa Adari, kuwa siku ya furaha na karamu, sikukuu ya kupelekeana zawadi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kutokana na sababu hii, Wayahudi wakaao vijijini na katika miji midogo huadhimisha siku ya kumi na nne ya mwezi wa Adari kuwa sikukuu ya furaha, na kupelekeana zawadi hali wale waishio katika miji mikubwa huadhimisha siku ya kumi na tano ya mwezi wa Adari kama siku ya mapumziko, wakapelekeana pia zawadi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndiyo sababu Wayahudi wanaokaa vijijini na katika miji midogo, huadhimisha siku ya kumi na nne ya mwezi wa Adari kama siku ya furaha na karamu, siku ambayo hupeana zawadi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndiyo sababu Wayahudi wanaokaa vijijini na katika miji midogo huadhimisha siku ya kumi na nne ya mwezi wa Adari kama siku ya furaha na karamu, siku ambayo wao hupeana zawadi mmoja kwa mwingine.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa sababu hii Wayuda wa mashambani wanaokaa katika miji iliyo wazi huifanya siku ya kumi na nne ya mwezi wa Adari kuwa siku ya furaha na ya karamu na sikukuu pia, nao hupeana matunzo mtu na mwenziwe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu hii Wayahudi wa vijijini, wakaao katika miji isiyo na boma, huishika siku ya kumi na nne ya mwezi wa Adari, kuwa siku ya furaha na karamu, sikukuu ya kupelekeana zawadi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kutokana na sababu hii, Wayuda wanaokaa katika vijiji na katika miji midogo wanasherehekea siku ya kumi na ine ya mwezi wa Adari kuwa sikukuu ya furaha, na kupelekeana zawadi wakati wale wanaoishi katika miji mikubwa wanasherehekea siku ya kumi na tano ya mwezi wa Adari kama siku ya mapumziko, na kupelekeana vilevile zawadi.