Esther 9:2 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Katika kila mji wa kila mkoa wa mfalme Ahasuero, Wayahudi walijiandaa vizuri kumshambulia mtu yeyote ambaye angejaribu kuwadhuru.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wayahudi walikusanyika katika miji yao, katika majimbo ya Mfalme Ahasuero kuwashambulia wale waliokuwa wanatafuta kuwaangamiza. Hakuna yeyote aliyeweza kushindana nao, kwa sababu watu wa mataifa mengine yote waliwaogopa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
siku ile ile Wayahudi wakakusanyika mijini mwao katika majimbo yote ya mfalme Ahasuero ili kuwatia mikono wale watu waliowatakia hasara; wala asiweze mtu kuwazuia, kwa kuwa hofu yao imewaangukia watu wote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Katika kila mji wa kila mkoa wa mfalme Ahasuero, Wayahudi walijiandaa vizuri kumshambulia mtu yeyote ambaye angejaribu kuwadhuru.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wayahudi walikusanyika katika miji yao, katika majimbo ya Mfalme Ahusuero kuwashambulia wale waliokuwa wanatafuta kuwaangamiza. Hakuna ye yote aliyeweza kushindana nao, kwa sababu watu wa mataifa mengine yote waliwaogopa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wayahudi walikusanyika katika miji yao, katika majimbo ya Mfalme Ahasuero kuwashambulia wale waliokuwa wanatafuta kuwaangamiza. Hakuna yeyote aliyeweza kushindana nao, kwa sababu watu wa mataifa mengine yote waliwaogopa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku hiyo ilipotimia, Wayuda wakakusanyika katika miji yao katika majimbo yote ya mfalme Ahaswerosi kuwaua kwa mikono yao waliotaka kuwafanyizia mabaya, lakini hakuwako mtu aliyesimama mbele yao, kwani mastusho yaliyaguia makabila yote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
siku ile ile Wayahudi wakakusanyika mijini mwao katika majimbo yote ya mfalme Ahasuero ili kuwatia mikono wale watu waliowatakia hasara; wala asiweze mtu kuwazuia, kwa kuwa hofu yao imewaangukia watu wote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika kila muji wa kila jimbo wa mufalme Ahasuero, Wayuda walijitayarisha vizuri kumushambulia mutu yeyote ambaye angejaribu kuwazuru.