Esther 9:22 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wayahudi waliwashinda maadui zao katika siku hizo, na katika mwezi huo huzuni yao iligeuzwa kuwa furaha, na misiba yao kuwa sikukuu. Waliagizwa wawe wakizikumbuka siku hizo kwa kufanya karamu na sherehe, kupelekeana zawadi za chakula na kuwapa maskini vitu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kama wakati ambao Wayahudi walipata nafuu kutoka kwa adui zao na kama mwezi ambao huzuni yao iligeuzwa kuwa furaha na kuomboleza kwao kuwa siku ya kusherehekea. Aliwaandikia kushika siku hizo kama siku za karamu na za furaha na kupeana zawadi za vyakula wao kwa wao na zawadi kwa maskini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ambazo ni siku Wayahudi walipojipatia raha mbele ya adui zao, na mwezi uliogeuzwa kwao kuwa furaha badala ya huzuni, na kuwa sikukuu badala ya kilio; wazifanye siku hizo ziwe za karamu na furaha, za kupeana zawadi na za kuwapa maskini vipawa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wayahudi waliwashinda maadui zao katika siku hizo, na katika mwezi huo huzuni yao iligeuzwa kuwa furaha, na misiba yao kuwa sikukuu. Waliagizwa wawe wakizikumbuka siku hizo kwa kufanya karamu na sherehe, kupelekeana zawadi za chakula na kuwapa maskini vitu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kama wakati ambao Wayahudi walipata nafuu kutoka adui zao na kama mwezi ambao huzuni yao iligeuzwa kuwa furaha na kuomboleza kwao kuwa siku ya kusherehekea. Aliwaandikia kushika siku hizo kama siku za karamu na za furaha na kupeana zawadi za vyakula wao kwa wao na zawadi kwa maskini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kama wakati ambao Wayahudi walipata nafuu kutoka kwa adui zao na kama mwezi ambao huzuni yao iligeuzwa kuwa furaha na kuomboleza kwao kuwa siku ya kusherehekea. Aliwaandikia kushika siku hizo kama siku za karamu na za furaha na kupeana zawadi za vyakula wao kwa wao na zawadi kwa maskini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kuwa sikukuu, kwa kuwa ndipo, Wayuda walipopata kutulia kwa adui zao; kwa hiyo ni mwezi, majonzi yao yalipogeuzwa kuwa furaha, nayo masikitiko yao kuwa siku nzuri. Kwa sababu hii wazifanye siku hizo kuwa za karamu na za furaha na za kupeana matunzo mtu na mwenziwe, nao wakiwa sharti wapelekewe vipaji.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ambazo ni siku Wayahudi walipojipatia raha mbele ya adui zao, na mwezi uliogeuzwa kwao kuwa furaha badala ya huzuni, na kuwa sikukuu badala ya kilio; wazifanye siku hizo ziwe za karamu na furaha, za kupeana zawadi na za kuwapa maskini vipawa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wayuda walishinda waadui zao katika siku hizo, na katika mwezi huo huzuni yao iligeuzwa kuwa furaha, na kilio chao kuwa sikukuu. Waliagizwa wakuwe wanazikumbuka siku hizo kwa kufanya karamu na sherehe, kupelekeana zawadi za chakula na kuwapa wamasikini vitu.