Esther 9:24 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hamani mwana wa Hamedatha, wa Agagi na adui wa Wayahudi alikuwa amefanya hila dhidi ya Wayahudi kuwaangamiza, pia alikuwa amepiga Puri, yaani kura, ili kuamua siku ya kuwaponda na kuwaangamiza Wayahudi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana Hamani mwana wa Hamedatha Mwagagi, adui wa Wayahudi wote, alikuwa amepanga hila dhidi ya Wayahudi ili kuwaangamiza, na alikuwa amepiga puri (yaani kura) kwa ajili ya maangamizi na uharibifu wao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kwa sababu Hamani bin Hamedatha, Mwagagi, adui ya Wayahudi wote, alikuwa amefanya shauri juu ya Wayahudi ili kuwaangamiza, akapiga Puri, yaani kura, ili kuwakomesha na kuwaangamiza pia;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hamani mwana wa Hamedatha, wa Agagi na adui wa Wayahudi alikuwa amefanya hila dhidi ya Wayahudi kuwaangamiza, pia alikuwa amepiga Puri, yaani kura, ili kuamua siku ya kuwaponda na kuwaangamiza Wayahudi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana Hamani mwana wa Hamedatha, Mwagagi, adui wa Wayahudi wote, alikuwa amepanga hila dhidi ya Wayahudi, kuwaangamiza na alikuwa amepiga puri (yaani kura) kwa ajili ya maangamizi na uharibifu wao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana Hamani mwana wa Hamedatha Mwagagi, adui wa Wayahudi wote, alikuwa amepanga hila dhidi ya Wayahudi ili kuwaangamiza, na alikuwa amepiga puri (yaani kura) kwa ajili ya maangamizi na uharibifu wao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani ndipo, Hamani, mwana wa Hamedata wa Agagi, aliyekuwa mpingani wa Wayuda wote, alipowazia kuwaangamiza Wayuda kwa hivyo, alivyokuwa amewapigia Puri, ndiyo kura, awatoweshe kwa kuwaangamiza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kwa sababu Hamani bin Hamedatha, Mwagagi, adui ya Wayahudi wote, alikuwa amefanya shauri juu ya Wayahudi ili kuwaangamiza, akapiga Puri, yaani kura, ili kuwakomesha na kuwaangamiza pia;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hamani mwana wa Hamedata wa ukoo wa Agagi na adui wa Wayuda alikuwa amefanya mupango juu ya Wayuda kwa kuwaangamiza, vilevile alikuwa amepiga purimu, ni kusema kura, kwa kuamua siku ya kuwaponda na kuwaangamiza Wayuda.