Esther 9:25 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Esta alipomwendea mfalme, naye mfalme alitoa amri kwa maandishi kwamba ile hila mbaya ambayo Hamani alikuwa amefanya dhidi ya Wayahudi, impate yeye mwenyewe; na ya kuwa yeye na wanawe wauawe kwa kutundikwa kwenye mti wa kuulia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini wakati shauri hilo baya lilipoarifiwa kwa mfalme, alitoa amri iliyoandikwa kwamba mipango mibaya ambayo Hamani ameipanga dhidi ya Wayahudi inapasa imrudie juu ya kichwa chake mwenyewe, na kwamba yeye na wanawe waangikwe mahali pa kunyongea watu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
bali mfalme alipoarifiwa, aliamuru kwa barua ya kwamba hilo shauri baya alilolifanya juu ya Wayahudi limrudie kichwani pake mwenyewe; na ya kwamba yeye na wanawe watundikwe juu ya mti.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Esta alipomwendea mfalme, naye mfalme alitoa amri kwa maandishi kwamba ile hila mbaya ambayo Hamani alikuwa amefanya dhidi ya Wayahudi, impate yeye mwenyewe; na ya kuwa yeye na wanawe wauawe kwa kutundikwa kwenye mti wa kuulia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini wakati shauri hilo baya lilipoarifiwa kwa mfalme, alitoa amri iliyoandikwa kwamba mipango mibaya ambayo Hamani ameipanga dhidi ya Wayahudi inapasa imrudie juu ya kichwa chake mwenyewe, na kwamba yeye na wanawe waangikwe mahali pa kunyongea watu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini wakati shauri hilo baya lilipoarifiwa kwa mfalme, alitoa amri iliyoandikwa kwamba mipango mibaya ambayo Hamani ameipanga dhidi ya Wayahudi inapasa imrudie juu ya kichwa chake mwenyewe, na kwamba yeye na wanawe waangikwe mahali pa kunyongea watu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mfalme alipopashwa habari hizo alikuwa ameagiza kwa barua kwamba: Wazo hilo baya, alilowawazia kuwafanyizia Wayuda, sharti limrudie kichwani pake, wamtundike yeye na wanawe mtini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
bali mfalme alipoarifiwa, aliamuru kwa barua ya kwamba hilo shauri baya alilolifanya juu ya Wayahudi limrudie kichwani pake mwenyewe; na ya kwamba yeye na wanawe watundikwe juu ya mti.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Esteri alipomwendea mufalme, naye mufalme akatoa amri kwa waandishi kwamba lile shauri baya ambalo Hamani alikuwa amefanya juu ya Wayuda, limurudilie yeye mwenyewe; na ya kuwa yeye na wana wake wauawe kwa kutundikwa kwenye muti.