Esther 9:27 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wayahudi waliifanya kuwa sheria rasmi kwao, kwa wazawa wao na kwa mtu yeyote ambaye angejiunga nao, kwamba katika wakati maalumu kila mwaka, bila kukosa, siku hizo mbili ziadhimishwe kulingana na maagizo ya Mordekai.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wayahudi wakachukua na kuimarisha desturi kwamba wao na wazao wao na wote ambao walijiunga nao wangezishika siku hizi mbili kila mwaka bila kuacha, kwa njia ilivyoelekezwa na kwa wakati wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wayahudi wakaagiza na kutadariki juu yao wenyewe, na juu ya wazao wao, na juu ya wote watakaojiunga nao, isikome, ya kwamba watazishika siku hizo mbili sawasawa na andiko lile, na kwa majira yake kila mwaka;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wayahudi waliifanya kuwa sheria rasmi kwao, kwa wazawa wao na kwa mtu yeyote ambaye angejiunga nao, kwamba katika wakati maalumu kila mwaka, bila kukosa, siku hizo mbili ziadhimishwe kulingana na maagizo ya Mordekai.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wayahudi wakachukua na kuifanya desturi kwamba wao na wazao wao na wote ambao walijiunga nao wangefanya bila kuacha kushika siku hizi mbili kila mwaka, kwa njia ilivyoelekezwa na kwa wakati wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wayahudi wakachukua na kuifanya desturi kwamba wao na wazao wao na wote ambao walijiunga nao wangefanya bila kuacha kushika siku hizi mbili kila mwaka, kwa njia ilivyoelekezwa na kwa wakati wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kwa kuyaitikia yale Wayuda wakaagiza, kwao nako kwao wa uzao wao nako kwao wote watakaojiunga nao iwe desturi isiyotanguka ya kuzishika hizo siku mbili hapo, siku zao zilizowekwa zitakapotimia kila mwaka utakaokuwa, kama yalivyoandikwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wayahudi wakaagiza na kutadariki juu yao wenyewe, na juu ya wazao wao, na juu ya wote watakaojiunga nao, isikome, ya kwamba watazishika siku hizo mbili sawasawa na andiko lile, na kwa majira yake kila mwaka;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wayuda wakaifanya kuwa sheria kwao, kwa wazao wao na kwa mutu yeyote ambaye angejiunga nao, kwamba katika wakati uliopangwa kila mwaka, bila kukosa, siku hizo mbili zishikwe kulingana na maagizo ya Mordekayi.