Esther 9:28 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Pia walikubaliana kwamba kila jamaa ya Kiyahudi, kizazi baada ya kizazi, katika kila mkoa na mji, sharti ikumbuke siku za Purimu na kuzisherehekea daima.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku hizi zinapasa zikumbukwe na kuadhimishwa katika kila kizazi, kila jamaa na katika kila jimbo na kila jiji. Nazo siku hizi za Purimu kamwe zisikome kusherehekewa na Wayahudi, wala kumbukumbu zake zisipotee miongoni mwa wazao wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
siku hizo zikumbukwe na kushikwa kwa vizazi vyote na kila jamaa, katika kila jimbo na kila mji; wala siku hizo za Purimu zisikome katikati ya Wayahudi, wala kumbukumbu lake lisiishe kwa wazao wao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Pia walikubaliana kwamba kila jamaa ya Kiyahudi, kizazi baada ya kizazi, katika kila mkoa na mji, sharti ikumbuke siku za Purimu na kuzisherehekea daima.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku hizi zinapasa zikumbukwe na kuadhimishwa katika kila kizazi, kila jamaa na katika kila jimbo na kila jiji. Nazo siku hizi za purimu kamwe zisikome kusherehekewa na wayahudi, wala kumbukumbu zake zisipotee miongoni mwa wazao wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku hizi zinapasa zikumbukwe na kuadhimishwa katika kila kizazi, kila jamaa na katika kila jimbo na kila jiji. Nazo siku hizi za Purimu kamwe zisikome kusherehekewa na Wayahudi, wala kumbukumbu zake zisipotee miongoni mwa wazao wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa sababu hii sikukuu hizi zikumbukwe, zishikwe kwa kila kizazi na kwa kila mlango katika kila jimbo na katika kila mji; hizo sikukuu za Purimu zisikome kabisa kwao Wayuda, wala ukumbusho wao usitoweke kwao wa uzao wao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
siku hizo zikumbukwe na kushikwa kwa vizazi vyote na kila jamaa, katika kila jimbo na kila mji; wala siku hizo za Purimu zisikome katikati ya Wayahudi, wala kumbukumbu lake lisiishe kwa wazao wao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vilevile walikubaliana kwamba kila jamaa ya Kiyuda, kizazi kwa kizazi, katika kila jimbo na muji, sharti ikumbuke siku za Purimu na kuzisherehekea siku zote.