Esther 9:29 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo malkia Esta, binti Abihaili, akaandika barua kwa mamlaka yake yote, pamoja na Mordekai Myahudi kuthibitisha yale aliyoandika Mordekai hapo awali kuhusu Purimu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Malkia Esta binti Abihaili, pamoja na Mordekai Myahudi, waliandika kwa mamlaka yote kuthibitisha barua hii ya pili kuhusu Purimu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo malkia Esta, binti Abihaili, pamoja na Mordekai Myahudi, alipoandika kwa mamlaka yote kuithibitisha barua hii ya pili ya Purimu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo malkia Esta, binti Abihaili, akaandika barua kwa mamlaka yake yote, pamoja na Mordekai Myahudi kuthibitisha yale aliyoandika Mordekai hapo awali kuhusu Purimu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Malkia Esta binti Abihaili, pamoja na Mordekai, Myahudi, waliandika kwa mamlaka yote kuthibitisha barua hii ya pili kuhusu Purimu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Malkia Esta binti Abihaili, pamoja na Mordekai, Myahudi, waliandika kwa mamlaka yote kuthibitisha barua hii ya pili kuhusu Purimu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Esteri, mkewe mfalme, mwana wa Abihaili, na Myuda Mordekai wakaandika barua ya pili na kuwashurutisha watu kwelikweli na kuwaagiza kuzishika hizo sikukuu za Purimu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo malkia Esta, binti Abihaili, pamoja na Mordekai Myahudi, alipoandika kwa mamlaka yote kuithibitisha barua hii ya pili ya Purimu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu malkia Esteri, binti ya Abihaili, akaandika barua kwa mamlaka yake yote, pamoja na Mordekayi Muyuda kuhakikisha ile Mordekayi aliyoiandika pale mbele juu ya Purimu.