Esther 9:31 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
na kuwahimiza wao na wazawa wao waadhimishe sikukuu za Purimu kwa wakati wake maalumu, kama vile walivyokuwa wanazikumbuka sheria za kufunga wakati wa kuomboleza. Maagizo haya yalitolewa na Mordekai, Myahudi, pamoja na malkia Esta.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
ili kuimarisha siku hizi za Purimu katika majira yake yaliyowekwa, kama Mordekai Myahudi na Malkia Esta walivyowaamuru, na walivyojiimarisha wenyewe na wazao wao kuhusu nyakati za kufunga na kuomboleza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ili kuzithibitisha siku hizo za Purimu kwa majira yake, kama Mordekai Myahudi na malkia Esta walivyoamuru, na kama walivyojiagizia juu yao wenyewe, na juu ya wazao wao, kwa habari ya kufunga na kilio.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
na kuwahimiza wao na wazawa wao waadhimishe sikukuu za Purimu kwa wakati wake maalumu, kama vile walivyokuwa wanazikumbuka sheria za kufunga wakati wa kuomboleza. Maagizo haya yalitolewa na Mordekai, Myahudi, pamoja na malkia Esta.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kuimarisha siku hizi za Purimu katika majira yake yaliyowekwa, kama Mordekai, Myahudi na Malkia Esta alivyowaamuru na walivyojiimarisha wenyewe na wazao wao kuhusu nyakati za kufunga na kuomboleza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
ili kuimarisha siku hizi za Purimu katika majira yake yaliyowekwa, kama Mordekai, Myahudi na Malkia Esta walivyowaamuru, na walivyojiimarisha wenyewe na wazao wao kuhusu nyakati za kufunga na kuomboleza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akaagiza kuzishika hizo sikukuu za Purimu siku zilezile, walizowaagiza Myuda Mordekai na Esteri, mkewe mfalme, kama walivyojiagizia wenyewe nao wa uzao wao mambo ya mifungo na ya maombolezo yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ili kuzithibitisha siku hizo za Purimu kwa majira yake, kama Mordekai Myahudi na malkia Esta walivyoamuru, na kama walivyojiagizia juu yao wenyewe, na juu ya wazao wao, kwa habari ya kufunga na kilio.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
na kuwaamuru wao na wazao wao washike sikukuu za Purimu kwa wakati wake uliopangwa, kama vile walivyokuwa wanazikumbuka sheria za kufunga wakati wa kuomboleza. Maagizo haya yalitolewa na Mordekayi, Muyuda, pamoja na malkia Esteri.