Exodus 1:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mnapowahudumia wanawake wa Kiebrania wanapojifungua, ikiwa mtoto anayezaliwa ni wa kiume, muueni. Lakini ikiwa ni wa kike, mwacheni aishi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mtakapowazalisha wanawake Waebrania, chunguzeni wanapojifungua. Ikiwa ni mtoto wa kiume, muueni; lakini ikiwa ni msichana, mwacheni aishi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
akasema, Wakati mwazalishapo wanawake wa Kiebrania na kuwaona wa katika kuzaa, ikiwa ni mtoto mwanamume, basi mwueni, bali ikiwa ni mtoto mwanamke, na aishi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mnapowahudumia wanawake wa Kiebrania wanapojifungua, ikiwa mtoto anayezaliwa ni wa kiume, muueni. Lakini ikiwa ni wa kike, mwacheni aishi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mtakapowazalisha wanawake wa Kiebrania wanapojifungua, chunguzeni; ikiwa ni mtoto wa kiume, mwueni; lakini ikiwa ni msichana, mwacheni aishi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mtakapowazalisha wanawake wa Kiebrania, chunguzeni wanapojifungua. Ikiwa ni mtoto wa kiume, muueni, lakini ikiwa ni msichana, mwacheni aishi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
akasema, Wakati mnapowazalisha wanawake wa Kiebrania na kuona kuwa ni mtoto wa kiume basi mwueni, bali ikiwa ni mtoto wa kike, na aishi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mnapowahudumia wanawake wa Kiebrania wanapojifungua, ikiwa mtoto anayezaliwa ni wa kiume, muueni. Lakini ikiwa ni wa kike, mwacheni aishi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kwamba: Mkiwazalisha wanawake wa Kiebureo waangalieni, wakizaa! Kama mtoto ni wa kiume, sharti mmwue, lakini kama mtoto ni wa kike, na apone!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
akasema, Wakati mwazalishapo wanawake wa Kiebrania na kuwaona wa katika kuzaa, ikiwa ni mtoto mwanamume, basi mwueni, bali ikiwa ni mtoto mwanamke, na aishi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Munapofanya kazi ya kuzalisha wanawake Waebrania, ikiwa mutoto anayezaliwa ni mwanaume, mumwue. Ikiwa ni mwanamuke, mumwache aishi.”