Exodus 1:19 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wao wakamjibu Farao, “Wanawake wa Kiebrania si sawa na wanawake wa Misri. Wao ni hodari; kabla mkunga hajafika, wao huwa wamekwisha jifungua.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakunga wakamjibu Farao, “Wanawake wa Waebrania ni tofauti na wanawake wa Misri; wao wana nguvu, nao hujifungua watoto kabla wakunga hawajafika.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wazalisha wakamwambia Farao, Ni kwa sababu hao wanawake wa Kiebrania si kama wanawake wa Kimisri; kwa kuwa ni hodari hao, nao huzaa kabla mzalisha hajapata kuwafikilia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wao wakamjibu Farao, “Wanawake wa Kiebrania si sawa na wanawake wa Misri. Wao ni hodari; kabla mkunga hajafika, wao huwa wamekwisha jifungua.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakunga wakamjibu Farao, “Wanawake wa Kiebrania ni tofauti na wanawake wa Kimisri; wao wana nguvu, nao hujifungua watoto kabla wakunga hawajafika.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakunga wakamjibu Farao, “Wanawake wa Kiebrania ni tofauti na wanawake wa Kimisri; wao wana nguvu, nao hujifungua watoto kabla wakunga hawajafika.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakunga wakamwambia Farao, Ni kwa sababu hao wanawake wa Kiebrania si kama wanawake wa Kimisri; kwa kuwa ni hodari hao, nao huzaa kabla mkunga hajapata kuwafikia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wao wakamjibu Farao, “Wanawake wa Kiebrania si sawa na wanawake wa Misri. Wao ni hodari; kabla mkunga hajafika, wao huwa wamekwisha jifungua.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao wazalishaji wakamwambia Farao: Ni kwa kuwa wanawake wa Kiebureo hawafanani na wanawake wa Kimisri, kwani wao wako na nguvu zaidi, mzalishaji akiwa hajafika bado kwao, wamekwisha kuzaa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wazalisha wakamwambia Farao, Ni kwa sababu hao wanawake wa Kiebrania si kama wanawake wa Kimisri; kwa kuwa ni hodari hao, nao huzaa kabla mzalisha hajapata kuwafikilia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wao wakamujibu mufalme wa Misri: “Wanawake wa Waebrania si sawa na wanawake Wamisri. Wao ni hodari; mbele muzalishaji hajafika, wao wanakuwa wamekwisha kuzaa.”