Exodus 1:22 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha Farao akawaamuru watu wake wote hivi, “Kila mtoto wa kiume atakayezaliwa kwa Waebrania mtupeni mtoni Nili. Lakini kila mtoto wa kike, mwacheni aishi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Farao akatoa agizo hili kwa watu wake wote: “Kila mtoto wa kiume atakayezaliwa kwa Waebrania lazima atupwe katika Mto Naili, bali kila mtoto wa kike aachwe aishi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha huyo Farao akawaagiza watu wake, akisema, Kila mtoto mwanamume atakayezaliwa mtamtupa mtoni, na kila mtoto mwanamke mtamhifadhi hai.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha Farao akawaamuru watu wake wote hivi, “Kila mtoto wa kiume atakayezaliwa kwa Waebrania mtupeni mtoni Nili. Lakini kila mtoto wa kike, mwacheni aishi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Farao akatoa agizo hili kwa watu wake wote: “Kila mtoto wa kiume atakayezaliwa kwa Waebrania lazima atupwe katika Mto Nile, bali kila mtoto wa kike aachwe aishi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Farao akatoa agizo hili kwa watu wake wote: “Kila mtoto wa kiume atakayezaliwa kwa Waebrania lazima atupwe katika Mto Naili, bali kila mtoto wa kike aachwe aishi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha huyo Farao akawaagiza watu wake wote, akisema, Kila mtoto wa kiume atakayezaliwa mtamtupa mtoni, na kila mtoto wa kike mtamhifadhi hai.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha Farao akawaamuru watu wake wote hivi, “Kila mtoto wa kiume atakayezaliwa kwa Waebrania mtupeni mtoni Nili. Lakini kila mtoto wa kike, mwacheni aishi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Farao akawaagiza watu wake wote kwamba: Kila mtoto wa kiume atakayezaliwa sharti mumtupe mtoni, lakini watoto wote wa kike na mwaache, wapone!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha huyo Farao akawaagiza watu wake, akisema, Kila mtoto mwanamume atakayezaliwa mtamtupa mtoni, na kila mtoto mwanamke mtamhifadhi hai.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha mufalme wa Misri akawaamuru watu wake wote hivi: “Kila mutoto mwanaume atakayezaliwa kwa Waebrania mumutupe ndani ya muto Nili. Lakini kila mutoto mwanamuke, mumwache aishi.”