Exodus 10:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Mose akainyosha fimbo yake juu ya nchi ya Misri. Mwenyezi-Mungu akaleta upepo toka mashariki, ukavuma juu ya nchi mchana kutwa na usiku kucha. Kulipokucha, ule upepo ukawa umeleta nzige.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo Musa akanyoosha fimbo yake juu ya Misri, Mwenyezi Mungu akauleta upepo wa mashariki ukavuma katika nchi yote mchana wote na usiku kucha, kufikia asubuhi upepo ukawa umeleta nzige.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Musa akainyosha fimbo yake juu ya nchi ya Misri, na Bwana akaleta upepo kutoka mashariki juu ya nchi, mchana kutwa, na usiku kucha; kulipopambazuka ule upepo wa mashariki ukawaleta nzige.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Mose akainyosha fimbo yake juu ya nchi ya Misri. Mwenyezi-Mungu akaleta upepo toka mashariki, ukavuma juu ya nchi mchana kutwa na usiku kucha. Kulipokucha, ule upepo ukawa umeleta nzige.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo Mose akanyosha fimbo yake juu ya Misri, BWANA akauleta upepo wa mashariki ukavuma katika nchi yote mchana wote na usiku kucha, kufikia asubuhi upepo ukawa umeleta nzige.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo Musa akanyoosha fimbo yake juu ya Misri, bwana akauleta upepo wa mashariki ukavuma katika nchi yote mchana wote na usiku kucha, kufikia asubuhi upepo ukawa umeleta nzige.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Musa akainyosha fimbo yake juu ya nchi ya Misri, na BWANA akaleta upepo kutoka mashariki juu ya nchi, mchana kutwa, na usiku kucha; kulipopambazuka ule upepo wa mashariki ukawaleta nzige.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Mose akainyosha fimbo yake juu ya nchi ya Misri. Mwenyezi-Mungu akaleta upepo toka mashariki, ukavuma juu ya nchi mchana kutwa na usiku kucha. Kulipokucha, ule upepo ukawa umeleta nzige.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mose alipoiinua fimbo yake juu ya nchi ya Misri, Bwana akaleta upepo toka maawioni kwa jua, nao ukavuma katika nchi hiyo mchana kutwa na usiku kucha; kulipokucha, huo upepo wa maawioni kwa jua ulikuwa umewaleta nzige.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Musa akainyosha fimbo yake juu ya nchi ya Misri, na BWANA akaleta upepo kutoka mashariki juu ya nchi, mchana kutwa, na usiku kucha; kulipopambazuka ule upepo wa mashariki ukawaleta nzige.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Musa akainua fimbo yake juu ya inchi ya Misri. Yawe akaleta upepo toka upande wa mashariki, ukavuma juu ya inchi muchana kutwa na usiku kucha. Kulipokucha, ule upepo ukaleta nzige.