Exodus 10:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hao nzige wakaenea kila mahali nchini Misri, wakatua juu ya ardhi yote. Nzige hao walikuwa kundi kubwa kupindukia, kiasi ambacho hakijapata kutokea wala hakitatokea tena.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakaivamia Misri yote na kukaa katika kila eneo la nchi kwa wingi. Kamwe halijapata kutokea pigo la nzige kama hilo, wala halitakuwa tena.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na hao nzige wakakwea juu ya nchi yote ya Misri, wakatua ndani ya mipaka yote ya Misri, walikuwa wabaya mno; hawajakuwapo nzige kama hao majira yo yote, wala baada yao hawatakuwa wengine jinsi hiyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hao nzige wakaenea kila mahali nchini Misri, wakatua juu ya ardhi yote. Nzige hao walikuwa kundi kubwa kupindukia, kiasi ambacho hakijapata kutokea wala hakitatokea tena.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakaivamia Misri yote na kukaa kila eneo la nchi kwa wingi. Kamwe hapajapata kuwepo pigo la nzige kama hilo, wala halitakuwepo tena.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakaivamia Misri yote na kukaa kila eneo la nchi kwa wingi. Kamwe hapajapata kuwepo pigo la nzige kama hilo, wala halitakuwepo tena.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na hao nzige wakakwea juu ya nchi yote ya Misri, wakatua ndani ya mipaka yote ya Misri, walikuwa wabaya mno; hawajakuwapo nzige kama hao majira yoyote, wala baada yao hawatakuwa wengine jinsi hiyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hao nzige wakaenea kila mahali nchini Misri, wakatua juu ya ardhi yote. Nzige hao walikuwa kundi kubwa kupindukia, kiasi ambacho hakijapata kutokea wala hakitatokea tena.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao hawa nzige wakaiingia nchi yote ya Misri, wakatua po pote katika mipaka ya Misri, nao walikuwa wakali sana wa kula; nzige kama hao walikuwa hawajatokea siku zilizopita, wala hawatatokea siku zijazo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na hao nzige wakakwea juu ya nchi yote ya Misri, wakatua ndani ya mipaka yote ya Misri, walikuwa wabaya mno; hawajakuwapo nzige kama hao majira yo yote, wala baada yao hawatakuwa wengine jinsi hiyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wale nzige wakaenea kila pahali katika inchi ya Misri, wakatua juu ya inchi yote. Nzige wale walikuwa kundi kubwa sana, kiasi ambacho hakijapata kutokea wala hakitatokea tena.