Exodus 10:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waliifunika nchi yote ya Misri, hata ardhi ikaonekana kuwa giza. Walikula mimea yote na matunda yote yaliyosalia wakati wa ile mvua ya mawe. Hakuna hata jani moja lililosalia nchini. Hakuna jani lolote lililosalia juu ya miti wala mimea popote katika nchi yote ya Misri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakafunika ardhi yote hata ardhi ikawa nyeusi. Wakatafuna kila kilichokuwa kimebakizwa na ile mvua ya mawe: kila kitu kilichoota shambani, pamoja na matunda kwenye miti. Hakuna kitu chochote cha kijani kilichosalia katika miti au mmea katika nchi yote ya Misri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa waliufunika uso wote wa nchi, hata nchi iliingia giza; wakala mimea yote ya nchi, na matunda yote ya miti yaliyosazwa na ile mvua ya mawe; hapakusalia hata jani moja, mti wala mmea wa mashamba, katika nchi yote ya Misri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waliifunika nchi yote ya Misri, hata ardhi ikaonekana kuwa giza. Walikula mimea yote na matunda yote yaliyosalia wakati wa ile mvua ya mawe. Hakuna hata jani moja lililosalia nchini. Hakuna jani lolote lililosalia juu ya miti wala mimea popote katika nchi yote ya Misri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakafunika ardhi yote mpaka ardhi ikawa nyeusi. Wakatafuna kile chote kilichokuwa kimebakizwa na ile mvua ya mawe, kila kitu kiotacho mashambani pamoja na matunda kwenye miti. Hakuna kitu cho chote cha kijani kilichosalia katika miti au mmea katika nchi yote ya Misri.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakafunika ardhi yote mpaka ardhi ikawa nyeusi. Wakatafuna kile chote kilichokuwa kimebakizwa na ile mvua ya mawe, kila kitu kiotacho mashambani pamoja na matunda kwenye miti. Hakuna kitu chochote cha kijani kilichosalia katika miti au mmea katika nchi yote ya Misri.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa waliufunika uso wote wa nchi, hata nchi iliingia giza; wakala mimea yote ya nchi, na matunda yote ya miti yaliyosazwa na ile mvua ya mawe; hapakusalia hata jani moja, mti wala mmea wa mashambani, katika nchi yote ya Misri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waliifunika nchi yote ya Misri, hata ardhi ikaonekana kuwa giza. Walikula mimea yote na matunda yote yaliyosalia wakati wa ile mvua ya mawe. Hakuna hata jani moja lililosalia nchini. Hakuna jani lolote lililosalia juu ya miti wala mimea popote katika nchi yote ya Misri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakaifunikiza nchi yote pia hapo juu, hata nchi ikapata giza; wakayala majani yote ya nchi nayo matunda yote ya miti, mvua ya mawe iliyoyasaza, hakukusalia jani moja tu penye miti wala penye vijiti vya mashambani katika nchi yote ya Misri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa waliufunika uso wote wa nchi, hata nchi iliingia giza; wakala mimea yote ya nchi, na matunda yote ya miti yaliyosazwa na ile mvua ya mawe; hapakusalia hata jani moja, mti wala mmea wa mashamba, katika nchi yote ya Misri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walifunika inchi yote ya Misri, hata inchi ikaonekana kuwa giza. Walikula mimea yote na matunda yote yaliyobaki wakati wa ile mvua ya mawe. Hakuna hata jani moja lililobakia katika inchi. Hakuna jani lolote lililobakia juu ya miti wala mimea popote katika inchi yote ya Misri.