Exodus 10:19 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye Mwenyezi-Mungu akaleta upepo mkali toka magharibi, ukawainua wale nzige na kuwasukumia kwenye bahari ya Shamu. Hakuna hata nzige mmoja aliyebaki katika nchi nzima ya Misri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Naye Mwenyezi Mungu akaugeuza upepo kuwa upepo mkali sana kutoka magharibi, ambao uliwaondoa wale nzige na kuwapeleka kwenye Bahari ya Shamu. Hakuna nzige hata mmoja aliyebaki popote katika nchi ya Misri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana akaugeuza upepo wa magharibi wenye nguvu nyingi, ambao uliwaondoa wale nzige na kuwapeleka katika Bahari ya Shamu; hakusalia hata nzige mmoja ndani ya mipaka yote ya Misri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye Mwenyezi-Mungu akaleta upepo mkali toka magharibi, ukawainua wale nzige na kuwasukumia kwenye bahari ya Shamu. Hakuna hata nzige mmoja aliyebaki katika nchi nzima ya Misri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Naye BWANA akaugeuza upepo ukavuma kutoka magharibi, wenye nguvu nyingi, ambao uliwaondoa wale nzige na kuwapeleka kwenye Bahari ya Shamu. Hakuna nzige hata mmoja aliyebaki po pote katika nchi ya Misri.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Naye bwana akaugeuza upepo ukavuma kutoka magharibi, wenye nguvu nyingi, ambao uliwaondoa wale nzige na kuwapeleka kwenye Bahari ya Shamu. Hakuna nzige hata mmoja aliyebaki popote katika nchi ya Misri.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA akaugeuza upepo wa magharibi wenye nguvu nyingi, ambao uliwaondoa wale nzige na kuwapeleka katika Bahari ya Shamu; hakusalia hata nzige mmoja ndani ya mipaka yote ya Misri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye Mwenyezi-Mungu akaleta upepo mkali toka magharibi, ukawainua wale nzige na kuwasukumia kwenye bahari ya Shamu. Hakuna hata nzige mmoja aliyebaki katika nchi nzima ya Misri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Bwana alipoleta upepo mwingine toka baharini wenye nguvu sana, ukawainua wale nzige, ukawapeleka na kuwatosa katika Bahari Nyekundu, asisalie nzige hata mmoja katika mipaka yote ya Misri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA akaugeuza upepo wa magharibi wenye nguvu nyingi, ambao uliwaondoa wale nzige na kuwapeleka katika Bahari ya Shamu; hakusalia hata nzige mmoja ndani ya mipaka yote ya Misri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye Yawe akaleta upepo mukali toka upande wa magaribi, ukawainua wale nzige na kuwasukumia kwenye bahari Nyekundu. Hakuna hata nzige mumoja aliyebaki katika inchi nzima ya Misri.