Exodus 10:24 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, Farao akamwita Mose, akamwambia, “Nendeni mkamtumikie Mwenyezi-Mungu. Watoto wenu pia wanaweza kwenda pamoja nanyi. Lakini kondoo na mbuzi, na ng'ombe wenu wabaki.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Farao akamwita Musa na kusema, “Nendeni, mkamwabudu Mwenyezi Mungu. Hata wanawake na watoto wenu mwaweza kwenda nao pia, lakini kondoo, mbuzi na ng’ombe wenu waacheni.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Farao akamwita Musa, na kumwambia, Haya, nendeni, mkamtumikie Bwana; kondoo zenu na ng'ombe zenu tu na waachwe; watoto wenu nao na waende pamoja nanyi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, Farao akamwita Mose, akamwambia, “Nendeni mkamtumikie Mwenyezi-Mungu. Watoto wenu pia wanaweza kwenda pamoja nanyi. Lakini kondoo na mbuzi, na ng'ombe wenu wabaki.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Farao akamwita Mose na kusema, “Nendeni, mkamwabudu BWANA. Hata wanawake na watoto wenu mwaweza kwenda nao pia, lakini kondoo, mbuzi na ng'ombe wenu waacheni.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Farao akamwita Musa na kusema, “Nendeni, mkamwabudu bwana. Hata wanawake na watoto wenu mwaweza kwenda nao pia, lakini kondoo, mbuzi na ng’ombe wenu waacheni.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Farao akamwita Musa, na kumwambia, Haya, nendeni, mkamtumikie BWANA; kondoo zenu na ng'ombe zenu tu na waachwe; watoto wenu nao na waende pamoja nanyi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, Farao akamwita Mose, akamwambia, “Nendeni mkamtumikie Mwenyezi-Mungu. Watoto wenu pia wanaweza kwenda pamoja nanyi. Lakini kondoo na mbuzi, na ng'ombe wenu wabaki.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Farao alipomwita Mose, akamwambia: Nendeni kumtumikia Bwana! Mbuzi na kondoo na ng'ombe tu waachwe huku, lakini wana wenu na waende nayi!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Farao akamwita Musa, na kumwambia, Haya, nendeni, mkamtumikie BWANA; kondoo zenu na ng’ombe zenu tu na waachwe; watoto wenu nao na waende pamoja nanyi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, mufalme wa Misri akamwita Musa, akamwambia: “Mwende mumutumikie Yawe. Watoto wenu vilevile wanaweza kwenda pamoja nanyi. Lakini kondoo na mbuzi, na ngombe wenu wabaki.”